Thursday, June 6, 2013

Nicki Minaj apata deal ya kuwa mmiliki mwenza na kisura wa wine mpya ‘Myx Fusion’

Baada ya hivi karibuni kutambulisha bidhaa yake mpya ya speaker alizozipa jina la ‘Pink Pill’ alizozitoa kwa ushirikiano na Beats by Dre, rapper wa kike Nicki Minaj ameendelea kupata deals za aina hiyo baada ya kusign deal ya kuwa face of ‘Myx Fusion’.

nicki-myx
Myx Fusion ni aina ya wine ambayo Nicki Minaj hatakuwa analipwa kama model tu wa bidhaa hiyo lakini pia ni mmiliki wa kushirikiana wa bidhaa hiyo mpya.
Akielezea furaha yake juu ya kinywaji hicho kupitia mtandao wa the ybf Minaj alisema “nina furaha kubwa kushirikiana na bidhaa ya Myx Fusion, sina shaka itakuwa namba moja, ina ladha nzuri na ni bidhaa bora ambayo watu wataipenda, na haitakuwa na ugumuu kuiuza. Myx fusions inatupa nafasi ya kuleta mapinduzi ya sekta ya mvinyo. ”
Chief marketing officer wa bidhaa hiyo alisema, “ushirikiano wa Nicki Minaj na Myx Fusion ni mchezo wa kubadilishana. Nicki ni mbunifu mwenye uwezo mkubwa wa kushawishi umma. Anabeba kila kitu kinachohusiana na Myx na kukiwakilisha kwa umma na kuleta mabadiliko, brand zote mbili Myx na Nicki vimeoana vizuri.”
Kwa sasa wine hiyo inapatikana New York, New Jersey, Los Angeles na Las Vegas, lakini inategemewa kuyafikia masoko mengine mbeleni.
Minaj anazidi kujiwekea nafasi nzuri ya kutengeneza pesa nje ya muziki kupitia brand ya jina lake kitu ambacho kinawanufaisha wasanii wengi wa Marekani kama Rihanna ambaye alizindua bidhaa ya lipstick hivi karibuni.

0 comments:

Post a Comment