Friday, June 7, 2013

JEZI MPYA KWA BAADHI YA TIMU ZA LIGI KUU ZA ENGLANG NA MASTAAA WAO WAKIWA WEMEZIVAA ANGALIA PICHA HIZO HAPA



WAKATI maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya England 'Barclays Premier League' yakishika kasi, klabu za ligi hiyo ziko katika hekaheka kali na ya aina yake ya kutambulisha jezi mpya za vikosi vyao kwa ajili ya msimu ujao ambao utaanza katikati ya Agosti, huku Man United ikiwa bingwa mtetezi.

Fuatana na clan infos kutambua aina hizo na maelezo yake kwa ufupi:
Cardiff City


Jezi zilizotengenezwa na Kampuni ya Puma zitakazovaliwa na timu ya Cardiff City itakapocheza dimba la nyumbani za msimu wa Ligi Kuu. Cardiff City ni kati ya timu tatu zilizopanda daraja.
Chelsea


'True Blues' David Luiz, Gary Cahill, Fernando Torres na Oscar wakionesha jezi za Chelsea msimu ujao.





Kutoka juu ni Juan Mata, Petr Cech, Fernando Torres na Oscar wakionesha jezi za msimu ujao za Chelsea.









Oscar akiwa ndani ya jezi mpya za Chelsea.



Jezi mpya za Chelsea zitakavyokuwa msimu ujao. Zimetengenezwa na Kampuni ya Adidas.





Juan Mata na David Luiz wakionesha jezi mpya za Chelsea msimu ujao.
Liverpool


Mshambuliaji Luis Suarez akipozi ndani ya uzi mpya wa Liverpool. Wengine ni Steven Gerrard na Pepe Reina.




Muonekano wa eneo la shingoni katika jezi mpya za Liverpool, ambazo zinafanana kwa kiasi kikubwa na zile za mwaka 1984 walizotwalia ubingwa wa Ulaya.





Jezi ya nyumbani ya Majogoo wa Jiji Liverpool kwa ajili ya msimu ujao.


Steven Gerrard, Pepe Reina na Luis Suarez wakionesha jezi za ugenini za Liverpool aka Wekundu wa Anfield.



Jezi mpya za Liverpool. Kutoka kulia ni Danny Sturridge, Steven Gerrard, Pepe Reina na Andy Johnson.
Manchester City


Jezi mpya za Man City itakavyokuwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya England.


Gael Clichy kulia akiwa na James Milner wakionesha jezi mpya za Man City.





Samir Nasri juu na James Milner chini wakionesha jezi mpya za Man City msimu ujao wa 2013/14.






Mlinda mlango wa Manchester City, Joe Hart akionesha jezi mpya za klabu yake.


Manchester United



Jezi mpya za nyumbani Old Trafford zitakazovaliwa na Man United msimu ujao wa Ligi Kuu ya England.










Juu inaonesha muundo wa 'collar' ya jezi mpya ya Man United msimu ujao, ambayo ina kifungo kimoja nyuma (kama kinavyoonekana) na vifungo viwili kwa mbele vya kuibana 'collar' (kama inavyoonekana) picha ya chini.
Newcastle United


Nyota Steven Taylor akionesha jezi za Newcastle United zitakazotumiwa msimu ujao katika mechi za ugenini.
Norwich City



Wachezaji wa Norwich City Bradley Johnson, Robert Snodgrass, Russell Martin na John Ruddy wakiwa ndani ya uzi mpya wa kikosi chao msimu ujao.


Vijana waokota mipira 'Ball Boys' wa Norwich City wakiwa ndani ya uzi mpya utakaotumiwa na timu yao msimu ujao.
Stoke City


Kushoto ni Peter Crouch akiwa na Robert Huth wakionesha jezi za msimu ujao za kikosi cha Stoke City.
Swansea City


Mfano wa jezi ya msimu ujao itakayotumiwa na kikosi cha Swansea City iliyotengenezwa na Kampuni ya Adidas.

West Ham United


Kushoto ni Matt Jarvis akiwa na jezi ya nyumbani ya West Ham United msimu ujao na kulia ni Kevin Nolan akiwa na jezi za ugeniniza Wagonga Nyundo hao wa jiji la London.

0 comments:

Post a Comment