Saturday, June 24, 2017

LUKAKU IN TANZANIA SOMA HAPA UJUE ZAIDI


Hakika hili ni swali ambalo kila mmoja wetu kwa sasa analiwaza akifikiria ujio wa klabu ya Everton ambao watakuja Tanzania mapema mwezi ujao.
Tayari ilishathibitishwa kwamba Lukaku hatakuwa na Everton katika msimu ujao wa ligi lakini hadi sasa Mbelgiji huyo hajasajiliwa na klabu yoyote ile.
Chelsea walitajwa kuongoza mbio za kumnunua Lukaku na tetesi zilisema wanakaribia kumsaini mshambuliaji huyo kwa dau la euro 100m lakini hadi sasa suala hilo limetawaliwa na ukimya.
Baadae Manchester United nao walionekana kuhamia kwa Lukaku baada ya uhamisho wa Antoine Griezman kushindikana lakini nao pia kama ilivyo kwa Chelsea hadi sasa hawajamsaini.
Inafahamika kwamba kikwazo kikubwa kumnunua Lukaku ni dau lake ambalo linakadiriwa sio chini ya euro 90 million, pesa zinazooenekana ni nyingi.
Manchester United wanamhitaji Lukaku kuziba nafasi ya Zlatan Ibrahimovich, Chelsea nao wanamuhitaji kuziba nafasi ya Diego Costa lakini hadi sasa wote wanaonekana kutoeleweka.
Bado wiki chache tu kampuni ya Sport Pesa iwalete Everton na watu wengi wanamsubiri Lukaku kuona kama atakuja au laa, hakika hili limatufanya kuvuta subira hadi siku hiyo Sport Pesa watakapowaleta Everton pale Temeke uwanja wa taifa.

0 comments:

Post a Comment