Monday, June 17, 2013

Albam ya Jay-Z kupatikana bure kwenye simu mpya milioni 1 za Samsung anga hapa kuona


Albam mpya ya Jay-Z Magna Carta Holy Grail,”itapatikana bure kwenye simu milioni moja za kwanza za Samsung Galaxy S3, Galaxy S4 na Galaxy Note 2 kwa wamiliki watakaodownload app maalum.
App hiyo itakayoanza kudownloadiwa June 24 inasemekana kutoa muonekano wa kwanza wa story binafsi na masuala yaliyochangia kutolewa kwa albam hiyo.
App hiyo itaizua (unlock) Magna Carta Holy Grail, July 4, siku 3 kabla haijaingia rasmi sokoni katika ulimwengu tofauti na Galaxy.
Ushirikiano huo wa Samsung na Jay-Z, ulianza rasmi kwa kuoneshwa tangazo la dakika tatu la televisheni jana usiku kwenye fainali za NBA.
The Wall Street Journal limeripoti kuwa Sumsung imelipia dola tano ambazo ni zaidi ya shilingi 8,000 kwa kila albam hizo milioni moja kuwapa bure wateja wake na kuifanya Magna Carta Holy Grail albam ya kwanza kwenda platinum hata kabla haijaingia sokoni

0 comments:

Post a Comment