Friday, May 31, 2013

Oprah Winfrey atunukiwa ‘Honorary Doctorate Degree’ kutoka Havard University



Mwanamke mwenye mafanikio makubwa kupitia talk show yake Oprah Winfrey, jana (May 30) akiwa katika vazi la joho ameongeza CV yake ya elimu baada ya kutunukiwa shahada ya uzamivu ya heshima (honorary doctorate) kutoka Harvard University.



Oprah shahada hiyo ya Doctor of Laws degree’, alitoa hotuba yake wakati wa kufuzu na kushare mambo kadhaa na wahitimu wenzake, ambayo mengi ni uzoefu wake hasa upande wa changamoto alizokuwa akikutana nazo katika safari nzima ya mafanikio ya career na maisha kwa ujumla.



“Haijalishi kwa kiasi gani unaweza kuwa juu … Katika hatua nyingine unakuwa mwenye mashaka, … Na wakati wa kufanya, kumbuka hili: hakuna kitu kama kushindwa. Kushindwa ni hali tu ya maisha kujaribu kukupeleka katika mwelekeo mwingine. ”

0 comments:

Post a Comment