Friday, May 31, 2013

Maskini Afrika yetu: Wanawake wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja waandamana kudai haki zao

Mengi kama haya tumekuwa tukiyasikia tukiyasikia yakitokea katika nchi zilizo bara la America na Ulaya, lakini sasa yameanza kutokea kwa nguvu zaidi katika bara letu lenye utamaduni wa kipekee na safi (Afrika) watu wanaojihusisha na mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja wameanza kupaza sauti hadharani kuomba vitendo vyao vipewe baraka na vyombo vya dola.

Huko nchini Afrika kusini wanawake wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (Lesbians) wamejitokeza hadharani kupinga sera za serikali ambazo hazizitambui haki zao wanazodai kuwa ni za msingi. Moja kati ya madai yao ni kutaka haki ya ndoa ya jinsia moja kuhalalishwa na pia waweze kurusiwa kuwa na wapenzi wao wa jinsia moja hadharani kama ilivyo kwa mapenzi tuliyozoea Africa kati ya watu wa jinsia tofauti.

Sera mapenzi ya jinsia moja lilianza kuwekwa hadharani na nchi za Ulaya kama Uingereza kwa kutaka kushinikiza nchi za Afrika kubariki swala la ushoga la sivyo Uingereza itasitisha misaada kwa nchi zitakazopinga.

Eeeh Mungu tuepushe na hii hali, njaa ya misaada isitupeleke shimoni.

0 comments:

Post a Comment