Saturday, July 20, 2013

Lulu achat na fans wake na kutoa tahadhari kwa wanaochat nae 'facebook’, apewa ushauri mzito..na kuhusu kurudi shule?Find out






Muigizaji maarufu mwenye umri mdogo Elizabeth Michael a.k. Lulu amepata muda wa kuchat na mashabiki wake kupitia fan page ya East Africa Television na amejitahidi kujibu baadhi ya maswali yao huku akipokea ushauri mzito.


Japokuwa maswali mengi hayakupata nafasi ya kujibiwa kitu kilichowafanya baadhi ya fans hao kupandisha ‘mori’ sometimes, lakini yapo mengi ambayo yalipata majibu pia.



Lulu akichat na fans wake

Moja kati ya swali liliulizwa ni kuhusu safari yake ya maisha ya shule ambayo yaliishia somewhere kwa muda..na hapa fan wake alitaka kujua ataendelea lini na safari hiyo!


“watc are yor planz ov going back 4 sculing jaman??????????/” aliandika Kelly Triney.


“am on process...soonmpnz nitarudi darasani.” Alijibu Lulu


Lakini Lulu amekuwa kwenye vichwa vya habari mara kwa mara hata kabla hajapata matatizo(…), hiyo ilikuwa point ya msingi ya kuanzia kwa fan wake anaejulikana kama Nyato Halici.



“Unajihisije ulivyo maarufu alaf unaandamwa na skendo?”


“kiukweli sijisikii vzuri...lakn najitahidi kuzikwepa.” Alijibu Lulu




Kwa upande mwingine wapo fans waliompa ushauri wa mzito msanii huyo huku wakielekeza points zao za msingi kwenye mlango wa imani na kumtegemea Mungu, huu ni baadhi ya ushauri.


Goodhope Maringo: Lulu mm nikiwa kama kaka yako.napenda kukushauri watu kukupenda bado wanakupenda na wengine wasiokupenda hakikisha unawarudisha kwa matendo mazuri na yakuigwa.kuvaa uchi na magazeti sasa basi umefanya mengi sasa ishi ukimtumainia mungu,bado we nimsichana mdogo unalakuifanyia jamii iki ikukumbuke mara utapokua hapo nao tena.jichunge na ujue si weng wanafuraha nawe nakutakia maisha marefu.ni mm goodhope maringo mshabki wako


Lucy Mlaponi : mdogo wangu napenda sana kazi zako, ushauri wangu mimi maisha yako mkabidhi yesu, atakufundisha, kukuongoza kwa kila jambo.


Keily Klair : kip up the spirit of a good actor my dear and avoid publicty & mediaz live a private life and a normal one.




Mwisho Lulu ambae ni moja kati ya wasanii wa kike wenye mvuto na wanao-make headlines na ku-attract attention ya watu wengi akatoa shukurani na angalizo.


“asanteni sana mashabiki wangu....naomba radhi kwa wale nilioshindwa kujibu maswali yenu...kiukweli maswali yalikuwa mengi na nimejitahidi kujibu baadhi ya maswali....account hii nilikuwa naitumia kwa muda tu,baada ya hapa haitakuwepo tena na wala sina account nyingine yoyote facebook...kuweni makini na ma lulu fake...asanteni sana...mbarikiwe...cheers.”


Lulu alitumia akaunti yenye nickname ya ‘hotlulu Michael’..zipo akaunti nyingi sana zenye jina kama hilo ama jina linaoonesha kuwa na uhusiano na Elizabeth Michael, na zote zimepambwa na picha zake, so take care kama unachat na Lulu facebook inaweza kuwa ni changa la macho sio the one.

0 comments:

Post a Comment