Friday, June 14, 2013

Video:Wimbo mpya wa Kanye West ‘I am a God’ ni Utata mtupu,ajifananisha na..! "I talked to Jesus, he said what up Yeezus"








Hivi Kanye West anautani na Mungu? Huenda hili likawa ni swali ambalo linaweza kujitokeza miongoni mwa waamini wengi hasa waliozama ndani katika maswala ya kidini watakapousikia wimbo mpya wa Rapper Kanye West ‘I am a God’ ambao upo katika album yake aliyoipa jina ‘Yeezus’.


Yeezy ameachia teaser ya wimbo huo kwa kuweka kipande cha video kinamuonesha akiwa studio na producer Rick Rubin akiurekodi wimbo huo.


Ukiacha mbali utata wa tafsiri ya jina la wimbo huo “I am a God”, jina la album Yeezus ambalo linasound kama…,kipande cha mashairi ya wimbo huo kinaweza kumfanya msikilizaji hasa mwenye imani ya dini flani (confidential) ajiulize lile swali.


Kanye anasema aliongea na Yesu, lakini maongezi yao yanakupa picha kama vile ni mazungumzo kati ya mtu na mshikaji wake wa karibu, yaani kama alikuwa anaongea na Jay-Z.


Siingii sana kwenye imani, lakini naijengea picha mitazamo ya baadhi ya watu katika hili, ila kwa wengine inaweza kuwa sio big deal.


Hiki ni kipande cha mashairi hayo: "I just talked to Jesus/ He said, 'What up, Yeezus?'/ I said, 'Sh**, I'm chillin'/ Tryin' to stack these millions/ I know he's the most high/ But I am a close high."



Album ya Kanye West ‘Yeezus’ itaingia sokoni June 18 mwaka huu ikiwa na nyimbo kumi.

bonyeza hapa kuona

0 comments:

Post a Comment