Monday, April 22, 2013

VIDIO IKIONYESHA JINSI WALIVYO KAMATA MTUHUMIWA WA UGAIDI NA WA ULIPUAJI WA MABOMU BOSTON .WAMESEMA ALIKUA ANAMIPANGO YA KULIPUA BOMU LINGINE






Polisi wa Massachusetts Marekani wametoa video inayoonesha jinsi wallivyoweza kumkamata mtuhumiwa wa pili wa ugaidi anaeaminika kuwa amehusika na ulipuaji wa mabomu Boston Marekani April 15.



Kamishna wa Polisi wa Boston Ed Davis amesema kuwa mtuhumiwa huyo ambae ni ndugu wa mtuhumiwa wa kwanza ambae alipoteza maisha alijipanga kulipua sehemu nyingine tena kwa sababu waligundulika kuwa na mabomu takribani sita pamoja na silaha nyingine ndogondogo.


Mtuhumumiwa huyo anaejulikana kwa jina la Dzhokhar alikamatwa usiku wa April 19 baada kukimbizwa na polisi akiwa na kaka yake Tamerlan na kutokana na kurushiwa risasi na polisi Tamerlan aliuawa. Kamishna wa Polisi wa Boston amesema mission yote ilipangwa na FBI ambao walianza kuwasaka watuhumiwa hao wawili ambao ni mtu na kaka yake wa tumbo moja.


Hali ya kiafya ya mtuhumiwa huyo ni mbaya sana kiasi kwamba ameshindwa kuongea na kuhojiwa hivyo bado zinafanyika jitihada zaidi kumpa tiba ili ahojiwe na kutoa taarifa zaidi.

0 comments:

Post a Comment