Monday, April 22, 2013

BEYONCE APIGWA NA SHABIKI WAKE KWENYE TAMASHA NA WAMVUTA NYWELE








Queen Beyonce anaendelea na tour yake ya Mrs. Carter World, lakini hivi karibuni video ya tamasha lake akiwa Belgrade Serbia imeingia katika mtando huku ikionesha hali ngumu aliyokutana nayo mwimbaji huyo ikiwa ni pamoja na kukutana uso kwa uso na kibao cha shabiki aliyekuwa miongoni mwa umati wa watu.







Video hiyo inaonesha Beyonce akipenya katikati ya umati mkubwa wa mashabiki akiwa anasindikizwa na bodyguard wake kuelekea jukwaani, na hapo alikumbana na mikono kadhaa ya mashabiki ikiwa ni pamoja na mkono wa shabiki ambae alimpiga kibao.



Sio kibao tu alichoambulia lakini pia Beyonce alipata wakati mgumu kupenya katikati ya mashabiki walio na hamu ya kumgusa japo nguo tu, wapo waliomvuta nywele. Lakini Beyonce aliweza kufika mwisho wa msafara huo. Video hiyo inaonesha tamasha alilofanya April 15 huko Serbia.



Angalia video ya tukio hilo

0 comments:

Post a Comment