Tuesday, March 5, 2013

‘Sitamsainisha msanii yeyote hadi P-Square wakiacha kuimba’– Jude Okoye


d9ec60506b1611e2b3e122000a1f9a4f_7
 CEO wa Northside Entertainment/Square Records, Jude Okoye ambaye ni kaka yao Peter na Paul Okoye wa kundi la P-Square la Nigeria amesema hana mpango wa kumchukua msanii yeyote katika lebo hiyo siku za usoni.

Muongozaji huyo wa video aliyejishindia tuzo kibao ameliambia jarida la Hiphop World kwenye interview, ’Sijui kuhusu Peter na Paul lakini mimi binafsi sitasaini msanii yeyote mpaka P-Square watakapoacha kuimba, kitu kile kile nilichokisema uliponiuliza kwanini huwa sifanyi video za wasanii wengine, kila mtu atakayekuja kwenye mwavuli huu ataanza kulinganisha.’
Aliongeza kuwa aliamua kufanya video za P-Square pekee ili kuepuka uwezekano wa wasanii wengine kudai anawapendelea wadogo zake zaidi. Mwaka jana Square Record ilimchukua msanii nje ya ukoo huyo, May D ambaye hata hivyo walimtimua

0 comments:

Post a Comment