This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Friday, February 3, 2017

Mourinho amtupia kijembe Klopp.



Jose Mourinho ni kocha asiyeishiwa na visa kila siku.Jana timu yake ya Manchester United walicheza dhidi ya Hull City mchezo ulioisha kwa suluhu ya bila kufungana.Na sasa kocha huyo kama kawaida yake hakuweza kukaa kimya amewajia juu waamuzi.
Mourinho anaamini maamuzi ya waamuzi wengi wa ligi kuu Uingereza huwa ni tofaufi kwa timu yake.Kauli ambayo inaweza kumtia matatani Mreno huyo kwa mara nyingine tena katika ligi kuu ya Uingereza.
Mourinho alisema “naona sheria kwangu ni tofauti na kwa wenzangu,sitaki kuongea sana kwa kuwa nalipa sana faini kuliko watu wengine na naadhibiwa sana kuliko watu wengine”.Jose hadi sasa ndiye kocha anayeongoza kuadhibiwa na marefa nchini Uingereza.
Hakuishia hapo Mourinho aliamua kumtupia kijembe kocha wa Liverpool Jurgen Klopp.Katika mchezo wa Liverpool dhidi ua Chelsea Klopp alionekana kumpayukia mwamuzi wa pembenj lakini hakuadhibiwa.Baadae Klopp alijitetea akisema hakumuambia neno baya bali alimwambia “hakuna awezaye kutufunga”.
Mourinho anasema “mmeona mechi ya jana kocha anamfokea muamuzi halafu muamuzi anamuambia kocha anapenda hisia zake,leo mimi katika mazingira yaleyale kama ya jana ninaaambiwa kaa chini au uende jukwaani”.Mourinho alionekana mwenye jazba kubwa baada ya timu yake kunyimwa penati. Matokeo ya sare ya jana yanaifanya timu ya Manchester United kubaki katika nafasi ya 6 huku pengo lao la pointi na alieko juu likizidi kuongezeka kwa alama 5

Hazard anazihofia timu hizi mbili tu kwenye mbio za ubingwa.



Chelsea wanaongoza ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama 56,Totenham wako nafasi ya pili wakilingana pointi na Arsenal walioko nafasi ya tatu wakiwa wote na pointi 47.Liverpool wako nafasi ya 4 na alama 46 sawa na Man City nafasi ya 5 na alama 46 huku Manchester United wakiwa nafasi yao ya 6 na alama zao 42.
Lakini mshambuliaji wa Chelsea hawaogopi Tottenham wala Liverpool wala Man City.Eden Hazard anawaogopa sana Manchester United na Arsenal anaziona ndio timu tishio katika safari ya ubingwa.Hazard anawaona United walioko nafasi ya 6 wanaweza kuchupa hadi kuwakaribia kwani tofauti kati ya United na Tottenham ni alama tano tuu.
Kauli hii inakuja siku chache kabla ya Chelsea kuwakabili Arsenal,”United walifanya vibaya raundi ya kwanza lakini siku za usoni wanacheza vizuri sana,wana kocha mzuri na timu yao ni bora sana nadhani wanakuja kwa spidi kubwa sana” aliongea Hazard wakati wa mahojiano na Thiery Henru ambae ni mchambuzi wa soka katika kituo cha Sky Sports.
“Tottenham ni wazuri sana lakini kwangu uzoefu wa Manchester United naona unaweza kuwafanya tuwahofie kwa sasa”,aliongeza Hazard.Hazard anaamini uzoefu wa United na Arsenal unaweza kuwa hatari zaidi kwao katika kipindi hiki cha mwisho cha kuusaka ubingwa.
Kuhusu makocha wawili Conte na Mourinho.Hazard anaamini Conte ana mbinu sana kwani muda mwingi mazoezini amekuwa akiwapa mazoezi ya kimbinu zaidi tofauti na Mourinho ambae hawakuwa wanafanya vitu vingi ila alikuwa akiwaamini wachezaji wake kwa kuwa wanajua cha kufanya.Hazard anasema kwa sasa anafurahia mbinu za Conte kwa kuwa anampa sana nafasi kushambulia.

Tuesday, January 31, 2017

Donald Trump amfuta kazi mwanasheria mkuu



Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi kaimu mwanasheria mkuu Sally Yates saa chache tu baada ya kuwaagiza mawakili wa idara ya haki nchini humo kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo raia wanaotoka katika baadhi ya mataifa ya kiislamu.

Taarifa ya Ikulu ya Whitehouse imemshtumu kwa usaliti.

Sally Yates ambaye aliteuliwa na Obama alisema kuwa hafikirii kwamba marufuku hiyo ya muda kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu ni halali.


Wadhfa wake umechukuliwa na kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kijimbo huko Virginia Dana Boente.

Agizo hilo la rais lililotiwa saini Ijumaa iliopita limesababisha maandamano nchini Marekani na ughaibuni.

Awali kundi moja la wanadiplomasia liliandika barua likikosoa agizo hilo wakisema litazidi kuhatarisha usalama wa taifa hilo.

WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA KATIKA MKUTANO WAO WA 28 JIJINI ADISI ABABA ,ETHIOPIA




Picha ya pamoja ya wakuu wa nchi za umoja wa Afrika katika mkutano wao wa 28 jijini Addis Ababa, Ethiopia. Rais Dkt John Pombe Magufuli ni wa pili mstari wa pili kulia.

Monday, January 30, 2017

VIDEO: Mane ameiangusha Senegal AFCON 2017










Striker wa Liverpool Sadio Mane alikosa mkwaju muhimu wa penati uliopelekea timu yake ya taifa ya Senegal kusukumwa n je ya Kombe la mataifa ya Afrika na Cameroon kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa penati 5-4.


Mane ambaye ni mchezaji ghali zaidi wa kiafrika, penati yake ilipanguliwa na golikipa wa Cameroon Fabrice Ondoa, kabla ya Vincent Aboubakar kupachika penati ya ushindi kwa Cameroon.


Senegal ilikuwa na nafasi ya kushinda game hiyo katika muda wa kawaida lakini umahiri wa golikipa wa Cameroon Fabrice Ondoa ulikuwa kikwazo kikubwa kwa Simba wa Teranga na kushuhudia pambano hilo likifika hadi dakika 120 bila timu hizo kufungana.


Matokeo hayo yanamaanisha sasa Mane anatarajia kurejea haraka kuungana na klabu yake ya Liverpool ambayo ilichezea kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa Wolverhampton Wanderers Jumamosi kwenye mchezo wa FA Cup raundi ya nne.


Mchezo kati ya Senegal na Cameroon ulikuwa unazikumbusha timu hizo mchezo wao wa miaka 15 iliyopita ambapo zilikutana kwenye fainali huko nchini Mali.


Kwenye fainali hiyo, Cameroon iliifunga Senegal kwa magoli 3-2 kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 120 kumalizika bila mshindi.


Cameroon inataraji kucheza nusu fainali na mshindi wa mechi ya robo fainali kati ya Democratic Republic of Congo au Ghana siku ya Alhamisi kutafuta timu itakayofuzu kucheza fainali .

Hawa ndio mabigwa na wamepiga pasi nyingi hadi sasa kwenye ligi 5 kubwa Ulaya angalia rekodi zao na assist na timu wanazochezea









Cesc Fabregas,Kelvin De Bruyne na Andre Iniesta ni wachezaji wanaosifika kupiga sana pasi.Lakini msimu huu hawapo hadi sasa katika orodha ya waliopiga pasi nyingi.Lakini Paul Pogba,Herrera na Henderson ni wachezaji waliopo kwenye listi hii.Hembu tuone wachezaji 10 waliopiga pasi nyingi katila ligi 5 kubwa barani Ulaya.
10.Benjamin Andre.
Timu Rennes
Pasi alozopiga 1181
Pasi za kwenda mbele 671
Nafasi alizotengeneza 22
Assist 2
9.Ander Herrera
Timu Man United.
Pasi alizopiga 1185
Pasi za kwenda mbele 691
Nafasi alizotengeneza 25
Assist 3
8.Marco Verrati.
Timu Psg.
Pasi alizopiga 1192
Pasi za kwenda mbele 719
Nafasi alizotengeneza 22
Assist 2
7.Malang Sarr
Timu Nice.
Pasi alizopiga 1237
Pasi kwenda mbele 953
Nafasi alizotengeneza 3
Assist 1
6.Thiago Alcantara
Timu Bayern Munich
Pasi alizopiga 1258
Pasi kwenda mbele 727
Nafasi alizotengeneza 25
Assist 3.
5.Wylan Cyprien
Timu Nice.
Pasi alizopiga 1260
Pasi za kwenda mbele 729
Nafasi alizotengeneza 23
Assists 3
4.Paul Pogba
Timu Manchester United.
Pasi alizopiga 1271
Pasi za kwenda mbele 760
Nafasi alizotengeneza 41
Assists 3
3.Marek Hamski
Timu Napoli.
Pasi alizopiga 1477
Pasi za kwenda mbele 713
Nafasi alizotengeneza 45
Assist 7
2.Jordan Herndeson
Timu Liverpool.
Pasi alizopiga 1533
Pasi za kwenda mbele 926
Nafasi alizotengeneza 28
Assists 4
1.Thiago Motta
Timu PSG
Pasi alizopiga 1623
Pasi za kwenda mbele 1148
Nafasi alizotengeneza 10
Assists 0

Asubuhi hii Mafundi wa TRL waliokesha wakitengeneza reli palipoanguka Treni








Treni ya abiria ya EXPRESS ikitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam January 29 2017 ilipata ajali maeneo ya Ruvu mkoani wa Pwani ambapo jioni yake timu ya Mafundi pamoja na viongozi wa shirika la Reli Tanzania iliwasili kwenye eneo la tukio.


Shirika la reli Tanzania TRL jana usiku lilifanya mahojiano katika eneo la tukio ambazo


Kwenye mahojiano hayo ilitamkwa kwamba reli hiyo iliyoharibika ni lazima itengenezwe ili kuruhusu Treni za Mizigo na abiria ziendelee na shughuli zake kama kawaida leo na ndio maana Mafundi hawa wamekesha wakitengeneza, unaweza kuwatazama kwenye hii video fupi hapa chini. source millardayo.com

Wednesday, January 25, 2017

UPDATE ZA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 25,2017





































Monday, January 23, 2017