Friday, February 3, 2017

Mourinho amtupia kijembe Klopp.



Jose Mourinho ni kocha asiyeishiwa na visa kila siku.Jana timu yake ya Manchester United walicheza dhidi ya Hull City mchezo ulioisha kwa suluhu ya bila kufungana.Na sasa kocha huyo kama kawaida yake hakuweza kukaa kimya amewajia juu waamuzi.
Mourinho anaamini maamuzi ya waamuzi wengi wa ligi kuu Uingereza huwa ni tofaufi kwa timu yake.Kauli ambayo inaweza kumtia matatani Mreno huyo kwa mara nyingine tena katika ligi kuu ya Uingereza.
Mourinho alisema “naona sheria kwangu ni tofauti na kwa wenzangu,sitaki kuongea sana kwa kuwa nalipa sana faini kuliko watu wengine na naadhibiwa sana kuliko watu wengine”.Jose hadi sasa ndiye kocha anayeongoza kuadhibiwa na marefa nchini Uingereza.
Hakuishia hapo Mourinho aliamua kumtupia kijembe kocha wa Liverpool Jurgen Klopp.Katika mchezo wa Liverpool dhidi ua Chelsea Klopp alionekana kumpayukia mwamuzi wa pembenj lakini hakuadhibiwa.Baadae Klopp alijitetea akisema hakumuambia neno baya bali alimwambia “hakuna awezaye kutufunga”.
Mourinho anasema “mmeona mechi ya jana kocha anamfokea muamuzi halafu muamuzi anamuambia kocha anapenda hisia zake,leo mimi katika mazingira yaleyale kama ya jana ninaaambiwa kaa chini au uende jukwaani”.Mourinho alionekana mwenye jazba kubwa baada ya timu yake kunyimwa penati. Matokeo ya sare ya jana yanaifanya timu ya Manchester United kubaki katika nafasi ya 6 huku pengo lao la pointi na alieko juu likizidi kuongezeka kwa alama 5

0 comments:

Post a Comment