Thursday, April 14, 2016

FC Barcelona imevuliwa Ubingwa wa UEFA na Atletico Madrid kwa kipigo hiki (+Video)





Usiku wa April 13 2016 ndio zilichezwa mechi mbili za mwisho za hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya, klabu ya FC Barcelona ilikuwa mgeni dhidi ya Atletico Madrid katika uwanja wa Vicente Calderon wakati FC Bayern Munich walikuwa Ureno kucheza na Benfica.


FC Barcelona ambao ndio walikuwa mabingwa watetezi wa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya, wamevuliwa ubingwa kwa kufungwa jumla ya 2-0, hivyo kuondolewa mashindano kwa jumla ya goli 3-2, hiyo inatokana na matokeo ya mechi yao ya Nou Camp kuifunga Atletico goli 2-1.





Magoli ya Atletico alifunga Antoine Griezmann dakika ya 36 na dakika ya 88 akapachika goli la pili kwa mkwaju wa penati na kufanya nyota wa FC Barcelona kama Lionel Messi na wengine kutoamini kilichotokea. FC Bayern wao wamepita kwa aggregate ya 3-2, baada ya mchezo wa leo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.


Video ya magoli ya Atletico Vs Barcelona, Full Time 2-0

1 comments: