Saturday, August 3, 2013

Hawa ndio wasanii wenye ushawishi zaidi Afrika Mashariki pengine... Watajwa kuwania tuzo ya Msanii/Kundi la mwaka Afrika Mashariki katika Nigeria Entertainment Awards 2013


  Katika kila dalili kuwa hawa ndio wasanii wanaoeleweka zaidi kutoka Afrika Mashariki, Orodha ya wasanii hawa ndio waliotajwa kutoka Afrika Mashariki ndani ya Naijeria Entertainment Awards 2013.



Goodlyf

Kwenye list kuna wakali....
Navio na kundi la Goodlyf kutoka Uganda, Kundi la P Unit na Camp Mulla kutoka Kenya, Fally Ipupa wa Kongo, K'Naan wa Ethiopia, hatua ambayo ni kiashirio kuwa ndio wakali wanaoeleweka zaidi kutoka Afrika Mashariki.


Wasanii hawa wanawania tuzo ya msanii, kundi la muziki la mwaka kutoka Afrika Mashariki.



K Naan



Kidum



Navio



P Unit



Fally Ipupa




Camp Mulla

Tukio kubwa kabisa la ugawaji wa tuzo hizi kwa washindi litafanyika Septemba Mosi mwaka huu huko New York Marekani ambapo mpaka sasa zoezi la upigaji kura kwa njia ya mtandao linaendelea.

Wasanii na makundi haya yaliyoingia katika kinyang'anyiro cha tuzo hizi wamekuwa na mafanikio na uwezo wa kipekee katika muziki, na hivyo kuwa mfano mzuri kwa wasanii wengine kufanya jitihada ili kuweza pia kuonekana na kazi zao kutambulika katika ngazi hizi za kimataifa

0 comments:

Post a Comment