Saturday, July 20, 2013

Kuhusiana na kesi ya Agnes Masogange, Soma hapa ujuwe mapya yaliyo ibuka


Ikiwa ni siku 16 tangu malkia wa video hapa 255, Agnes Masogange kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya huko Afrika Kusini, Gaziti moja la hapa Tanzania limeweza kuandika haya kuhusiana na update za kesi yake.

Gazeti hilo limesema, Chanzo chetu cha ndani kilichoongea na paparazi wetu juzi jijini Dar, kimesema neno kwa neno, hasa matukio ya siku nne wakati staa huyo akijiandaa kuondoka nchini. Masogange aliondoka Julai 5, 2013.

JULAI 2, 2013
Masogange alipika pilau nyumbani kwake, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam na kuwaalika watu mbalimbali, wakiwemo kaka zake ambao majina yao hayakupatikana mara moja. Katika ‘hafla’ hiyo, Masogange alisema amejisikia kula pamoja na watu hao ili kutimiza furaha ya moyo wake. Hakusema ana furaha gani.

JULAI 3, 2013
Inadaiwa Masogange siku hiyo aliazima gari la mdau wake mmoja (jina tunalo) na kuwa nalo kwa saa kadhaa. Safari yake kubwa ilikuwa Sea View Hotel, jijini. Siku hiyo staa huyo hakuwa akipokea simu asizozijua. Wale aliowajua aliwaambia ana mazungumzo nyeti na mtu hotelini hapo, hivyo wapige baadaye.

JULAI 4, 2013
Masogange aliposti picha kwenye Instagram akiwa yeye na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ wakila ‘bata’. Aliandika maneno mbalimbali kama; ‘libeneke la bata litaendelea nikirudi.’ Hakusema anakwenda wapi na lini atarudi.


MZIGO ULITOKEA BARA LA ASIA
Kwa mujibu wa maelezo ya mtu mwingine, mzigo aliokamatwa nao Masogange unadaiwa kuingia Bongo Juni 29, 2013 ukitokea nchi moja iliyopo Bara la Asia (jina tunalo). “Sina uhakika na lini mzigo huo uliingia au safari hiyo aliipanga, lakini kumbukumbu zangu zinaniambia mzigo uliingia Bongo Juni ishirini na tisa, mwaka huu, ukitokea nchini …(anaitaja jina),” alisema mtu huyo.

AKIPATIKANA NA HATIA ADHABU NI HII Habari kutoka chanzo chetu kimoja nchini Afrika Kusini, mtu anayepatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya kwa kuuza au kubeba huhukumiwa kifungo cha maisha au kifungo cha miaka 20.

DHAMANA IPO WAZI.
Habari mbaya ni kwamba, dhamana ya Masogange na mwenzake iko wazi mahakamani lakini watu wa kwenda mstari wa mbele kumuwekea ndiyo wamekuwa wakiingia mitini. “Huku dhamana iko wazi, ila kila mtu anaonekana kukwepa kumdhamini. Sijui watu wanadhani atatoroka? Lakini nijuavyo mimi hawezi kutoroka kwa sababu paspoti yake inashikiliwa na serikali,” alisema mnyetishaji wetu aliye nchini humo.






0 comments:

Post a Comment