Saturday, July 27, 2013

Haya ndio maajabu ambayo wala bata hawa wamewaachia polisi na kutokomea mbali huko Ujerumani






Polisi huko Ujerumani wamekutana na tukio hili ambalo lilikuwa jipya kidogo kwao katika utaratibu wao wa kila siku wa kazi baada ya kulazimika kusimamisha gari moja ya wazi aina na BMW, baada ya kuona ikimwanga maji katika namna ya kushangaza wakati ilipokuwa ikikata kona bararabani.





Officer huyu na watu wengine walioshuhudia tukio hili walishangazwa zaidi hasa baada ya kusogelea gari hii na kukuta likejazwa maji ndani yake katika mfumo wa bwawa la kuogelea (swimming pool) huku ndani yake kukiwa na watu watatu waliokuwa wamevaa mavazi yao ya kuogelea ambao walikimbia na kutelekeza gari hii baada ya kusimamishwa na polisi.

Kutoka katika taarifa ya uchunguzi, Gari hii ya ajabu iligundulika ilikuwa inaendeshwa na watu waliokuwa wamelewa na ikiwa na uwezo wa kwenda kwa mwendo wa kilomita 25 tu kwa saa, ikiwa haina kibali chochote cha kutembea barabarani.







0 comments:

Post a Comment