Monday, June 3, 2013

Wale ma funs wa the blues ,Jose Mourinho Athibitisha Kurudi Chelsea soma hapa mpango mzima

Kwenye mahojiano aliyofanyiwa weekend hii Kocha Jose Mourinho amethibitisha kuwa kabla ya mwisho wa wiki hii atakuwa kocha rasmi wa Chelsea. Jose amesisitiza kuwa upendo wa mashabiki wa Chelsea ndio umemfanya akubali tena kazi hio kiraisi zaidi. Kwenye kipindi cha Tv Cha Punto Pelota huko Spain Jumapili hii Jose amesema atakuwa London kumalizia makubaliano yake yakurudi Stamford Bridge. Game ya mwisho ya Mourinho na Real Madrid walishinda 4-2 dhidi ya Osasuna jumamosi hii. Kabla ya kwenda Real Madrid, Jose alifundisha Chelsea kwa miaka 4 na kuthibitisha uwezo wake kama manager.

Jose amesema " Naenda London Jumatatu na kabla ya mwisho wa wiki hii nitakua manager wa Chelsea, " Watu wa kule wananipenda na maisha yangu yatakuwa bora zaidi nikizungukwa nao" [Chanzo Soccer Net]

0 comments:

Post a Comment