Tuesday, June 4, 2013

Ujumbe mtamu wa K’Lyn kwa mpenzi wake ‘Reginald Mengi’ ni moja kati ya the sweetest messages in May







Kumekuwa maswali mengi kuhusu wapi alipo na anafanya nini mrembo aliyewahi kukimbiza katika medani ya muziki Tanzania na ngoma kali kama ‘Nishike Mkono’, namzungumzia Jackline Ntuyabaliwe a.k.a K’Lyn.


Lakini majibu yanaweza kujieleza kuwa.. She is taking care of big things, watoto wawili mapacha aliozaa na moja kati ya wajasiliamali waliofanikiwa zaidi na wenye heshima kubwa Afrika ambae ni mmiliki wa makampuni ya IPP Media, Regnald Mengi ni moja kati ya vinavyomkeep busy.


May 28 ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa Regnald Mengi (Birthday) na watu wengi walimtakia heri ya siku ya kuzaliwa a.k.a happy birthday kwa lugha ya kigeni. Lakini ujumbe laini wa mrembo K’Lyn ulikuwa tofauti kabisa na ujumbe wa watu wengine, na hii ni kutokana na ile intimate relationship kati yao.


Mrembo huyo alitumia akaunti yake ya Twittter kuuwambia ulimwengu jinsi anavyomthamini, kumpenda na kumjali baba wa watoto wake mapacha, na kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa.


“Today is very special!Its the birthday of the love of my life,my best friend and the father of my twins.Happy birthday my love @regmengi.”


Utakubaliana na mimi kuwa huu unaweza kuwa kati jumbe laini na tamu kwa mwezi huu May hasa zile zilizowekwa hadharani.


Kwa jina kubwa alilonalo na heshima kubwa aliyonayo bwana Mengi alipata jumbe za kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa toka kwa watu wengi duniani, na yeye aliwajibu baada ya kuipitisha siku yake ya kuzaliwa na kuwashukuru kwa lugha mbili, kikwetu (Kiswahili) na kiingereza.


“Nawashukuru sana wote mlionitakia Happy Birthday. Asanteni sana. Nawatakia afya njema, furaha na mafanikio katika yote mnayofanya.”


“My most sincere thanks to all who wished me a happy birthday. I wish u good health, happiness and great success in all that u do.”

0 comments:

Post a Comment