Saturday, June 8, 2013

Polisi wakimbia nyumbani kwa Michael Jackson baada ya kupata taarifa kuwepo shambulio la risasi





Michael Jackson na watoto wake walipokuwa wadogo

Familia ya Marehemu Michael Jackson inaanza tena kuwa sehemu ya vichwa vya habari vya magazeti mengi hasa nchini Marekani. Siku moja baada ya mtoto wa kike wa Michael ‘Paris Michael’ kunusurika katika jaribio la kujiua, polisi wa Los Angeles walilazimika kukimbia haraka nyumbani kwa familia ya Marehemu Michael Jackson baada ya kupata ripoti kuwa kulisikika milio ya risasi.




Ripoti zinasema Polisi walipigiwa simu na mtu mmoja aliyewajulisha kuwa kulikuwa na shambulio la risasi lakini baada ya kufika nyumbani hapo hawakukuta dalili zozote za kuwepo shambulio lolote na hali ilikuwa shwari.


“Tulienda hadi nyumbani kwao kuona kama kuna kitu, lakini hakukuwa na kitu chochote. Nyumba ile imekuwa na kazi nyingi za kufanya hadi mida usiku sana, kwa hiyo tulituma kikosi pale.” Alisema msemaji wa kitengo cha polisi wa Los Angeles,Steve Whitmore.

0 comments:

Post a Comment