Monday, June 3, 2013

Mwigizaji mkongwe afunguka, “Oral sex imenisababishia kansa ya koo na sio pombe na uvutaji sigara”






Michael Douglas na Mkewe Catheline Zeta-Jones


Kuna wakati mtu anaweza kuweka hadharani siri yake kwa nia njema ya kuokoa maisha ya watu wengine watokana na ushuhuda wake, na hii ni kwa kuwa watu wengi huwa wagumu wa kubadilika hadi waone mfano hai ama mtu aliyeathirika kutokana na tabia flani akitoa ushuhuda.




Muigizaji mkongwe mwenye umri wa miaka 68 Mmarekani Michael Douglas ameweka wazi kuwa tatizo lake la kansa ya koo lilisababishwa na tabia yake ya kufanya oral sex.


Nguli huyo wa filamu alifunguka alipofanyiwa mahojiano na gazeti la The Guardian la marekani ambapo alikanusha tetesi ambazo wengi walikuwa wanaziamini kuwa uvutaji wa sigara na ulevi ndio uliosababisha yeye kupata kansa ya koo.


Alisema ugonjwa alionao umetokana na maambukizi ya virusi vinavyojulikana kama Human papolloma Virus (HPV) ambavyo vinasababisha magonjwa ya zinaa.


Douglas aligundua kuwa na kansa ya koo august 210, na akaanza kufuata matibabu ambapo alipitia hatua nne, lakini pia akapitia matibabu ya kina (intensive course of chemotherapy and radiation), na kufikia january 2011 alikuwa ameweza kwa kiasi kikubwa kupambana na maradhi hayo.

0 comments:

Post a Comment