Friday, June 21, 2013

Chidi Beenz asema hajawahi kuwa na ugomvi na Kala Pina! Atapanda jukwaani leo kwenye show ya Kikosi cha Mizinga






Mkali wa Michano toka Ilala ‘Chidi Beenz’ amesema hajawahi kabisa kuwa na ugomvi na kiongozi wa Kikosi cha Mizinga Kala Pina na kwamba waandishi wa habari ndio waliandika vile wanavyojua kuhusu issue hiyo.


“Hatujawahi kuwa na ugonvi na Pina, ndo maana wewe ukiniuliza nimemaliza lazima nikuulize tumemaliza nini. Ni ninyi waandishi na watu wa habari mliamua kuandika vitu mnavyojua nyinyi hakuna ugomvi uliotokea,” Chid Benz aliuambia mtandao wa Bongo5.


Chidi atakuwa mmoja kati wasanii watakaotumbuiza kwenye show ya miaka 13 ya kikosi cha mizinga leo(June 21).


Akiongea katika kipindi cha power Break Fast cha Clouds Fm, Kala Pina amesema hakuna tena ugomvi kati yake na Chidi Benz na ndo sababu ataungana na Kikosi kwenye show yao.


Chidi Beenz na Kala Pina walizinguana katika show ya kikosi cha mizinga baada ya Chidi kupanda jukwaani na kutoa speech bila kuwa kwenye ratiba, kitu kilichomfanya Kala kumshusha kwa nguvu.

0 comments:

Post a Comment