Thursday, May 30, 2013

Kilio cha majirani wa Justin Bieber chasikika, gari lake lashikiliwa na polisi eneo hilo





Siku moja baada ya majirani wa mwimbaji Justin Bieber kupiga kelele za kuomba msaada kupitia vyombo vya habari wakimtuhumu mwimbaji huyo kugeuka kero na kuvuruga utulivu wa wa maeneo hayo kwa tabia yake ya kuendesha kwa kasi, kupiga kelele na kuvuta marijuana mbele ya watoto, kilio chao kimefika mbali na gari la msanii huyo limeingia kwenye mikononi ya polisi.


Ripoti zinasema gari la mwimbaji huyo aina ya Farrari lilisimamishwa na polisi nje kidogo ya geti la Bieber sababu ikiwa ni mwendo kasi uliopitiliza kwa kuzingatia kuwa yuko katika maeneo ya makazi ya watu. Lakini bahati nzuri Bieber mwenyewe hakuwa na gari hilo siku hiyo na lilikuwa linaendeshwa na rafiki yake aliyefahamika kwa jina la ‘Lil Twist’.

Lakini ripoti kutoka kwa chanzo cha kuaminika upande wa polisi ni kwamba baada ya mahojiano ya muda polisi hao walimpa onyo kijana huyo na kumruhusu aendelee na safari yake.


Hivi karibuni majirani zake Justin Bieber walilalamika na kutishia kumfungulia mashtaka kwa kuwa huwapigia kelele nyingi akiwa anarudi kutoka club na rafiki zake, lakini pia huendesha gari lake kwa kasi sana wakati yuko katika eneo la makazi ya watu, na tuhuma mbaya zaidi ni kwamba huvuta marijuana mbele ya watoto wao wenye umri wadogo.

0 comments:

Post a Comment