Tuesday, February 12, 2013

Kofia aliyovaa The-Dream yageuka kituko, Jay-Z aliidiss wakati anamshukuru Soma mpango mzima


Mavazi ya mastaa hasa wa kike katika matukio makubwa yanayowajumuisha mastaa wengi huwa yanaleta gumzo wakati mwingine na kumake headlines, lakini katika tuzo za Grammy zilizofanyika jumapili ilikuwa tofauti baada ya The Dream kutupia kofia ambayo watazamaji wengi waliitafsiri wanavyoweza, watazamaji wengi walionekana kuiangalia mara kwa mara na kwa mtazamo wa wengi ilikuwa inachekesha. 

 Wakati Jay-Z , Frank Ocean na The Dream wamepanda kupokea tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana “No Church in the Wild”, wote walizungumza kidogo, na ilipofika zamu ya Jay-Z alirusha diss kiaina kama sio utani kwa The Drem, “I want to thank the swap meet for his hat”, ukumbi mzima ukadodosha kicheko wakati The Dream akitabasam kiaina.

0 comments:

Post a Comment