Tuesday, February 26, 2013

50 C ENT APATA BAHATI TENA BAADA YA KUGUSA TUMBO LA AMBER ROSA





Kiongozi wa G-Unit Curtis Jackson a.k.a 50 Cent hivi karibuni amefunguka kuhusu mtoto wa Wiz Khalifa na Amber Rose ambae alipokelewa duniani na kupewa jina la Sebastian Taylor Thomaz.


Kwa mujibu wa Fif, alipata nafasi ya kupiga story na Rose na Wiz hata kabla hawajawa wazazi wa Sebastian wakati bado Sebastian yuko tumboni.



Katika interview aliyofanya na DJ Whoo Kid, 50 Cent alipoulizwa mtazamo wake kuhusu mtoto wa Wiz na Rose, kwanza aliwapa hongera sana na akafunguka zaidi, “ Oh yeah, congratulation, Unajua niliwafukuzia kwenye gas station, yap Sebastian, niligusa juu ya tumbo la Amber. Na kitoto kilinipa bahati nzuri. Na itakuwa ni bahati nzuri, Inabidi ufikirie kuhusu hili, mtoto hana nafasi ya kutenda dhambi.”


Mapema mwezi February, Wiz alitweet kuhusu 50 Cent kuonesha upendo kwa mtoto wao wakati bado Rose anaujauzito, tweet yake ilisomeka, “Cool sh*t that happens at the gas station: @50 Cent hops put shows love and rubs the baby #Awesome.”

Wiz na Amber Rose walimkaribisha mtoto wao duniani February 21, na celebs wengi waliwapongeza akiwemo uncle Snoop Dogg a.k.a Snoop Lion.

0 comments:

Post a Comment