Monday, January 21, 2013

MUZIKI | ROMA ANAENDELEA KUFANYA UFAFANUZI WA MISTARI YAKE NDANI YA "2030"


Mkali wa 2030, ROMA kupitia ukurasa wake wa facebook anaendelea kufanya ufafanuzi wa mashairi yake, yaliyo katika wimbo unaofanya vizuri wa 2030 aliomshirikisha chipukizi wa mziki STORI.
Na hapa ni moja ufafanuzi wa baadhi ya mistari yake iliyo katika wimbo huo........

UNAPEWA CONTENA LA CONDOMS UIHONGE DHAHABU
MV SPICE ILIPOZAMA TV INAONYESHA TAARAB

means-

tuliowaita wanyonyaji miaka ileeee...leo tumewabatiza na tunawaita wawekezaji na hatimaye tunawapa rasili mali za taifa, kwa misaada midogo midogo kama hiyo!!

Huo ni mfano tu...lakini utakuta nchi inatoa ardhi na baadhi ya rasilimali kwa vizinga mbali mbali kama vyandarua nk!! sawa ni mahitaji mazuri hayo tupewayo ingawaje TBS nao wana mapungufu yao ktk uhakiki wa misaada hii kama ipo sawia!!

Lakini sio kwa kutoa rasilimali za nchi!! ni sawa na KUUZA MTOTO WAKO UMPENDAE NA KUMTEGEMEA AAF WAO WAKULIPE KWA KUKUPA SUFURIA!! sawa utapikia lakini kweli ndo ugawe mtoto?

Kipindi cha maafa ya ajali ya meli ya mv spice kuzama...tazama wengi tulihangaika kujua chanzo cha ajali, wengi tulihangaika kujua nini kinaendelea ajalini na zoezi la uokoaji linaendeleaje!

Sasa imagine unasikia taarifa kuwa ajali kubwa kama hii ya maelfu imetokea, then unataka kujua nini kinaendelea unakimbilia kuwasha tv, tena pengine ni tv ya taifa then unakuta inapiga muziki(TAARAB).

Wakati kituo hicho nacho pia huchukua na kuendeshwa kwa kodi zetu sisi walalahoi, sasa si ni wajibu wetu na haki yetu kupata taarifa za msingi kama hizo kwa wakati husika? hujui kama kuna damu zetu ajalini kule? mbona al jazeera na bbc wanaweza kuyaishi haya!!!

SO MISTARI MIWILI KAMA HIYO TAFSIRI YAKE NI KAMA HIVYO!! NA INATAKIWA IZUE HOJA NYINGI HUKO MITAANI MAANA NDIPO HIP HOP ILIPOTOKEA NA INAWAKILISHA MITAA.

NA HOJA HIZO ZIWE KTK KUJENGA ILI IJE KUONEKANA HIP HOP IMELETA UKOMBOZI KIFIKRA, KIMAADILI, KIUONGOZI NA JAMII NA TAIFA KWA UJUMLA!!!

and thatz hip hop (MOVEMENT)kama hausapoti movement za masela basi usikae pia kwenye njia zetu masela oiii... du ua thingz homie !!


TANGA MMEKOSA NINI AMKENI ACHENI UMWINYI
HAWA WACHAGA HAWATUWEZI ONA MANKA BARA 20

Means-

Tanga ni jiji sasa, lakini kutokana na asili yake kuna tabia ua umwinyi, wakazi wake wengi ambao ni wazawa wana tabia hizo, mdigo anafungua duka saa 5 au 6 imagine!! na sio kama alikuwa ana majukumu sijui NO!! basi tu hana hata sababu, ukiuliza atakwambia aaaah hata nkiwahi hamna wateja na hapo ikifika saa 7 ataenda kuswali!! sawa yuko sahihi dua muhimu!!, utakuta saa 12jioni kafunga duka karudi kwake, sasa ATAPATAJE MAENDELEO HUYU MTU?!!!

Wakati huo kuna mtu hadi saa 5 asubuhi kashaingiza hela ndefu tu kwa uuzaji huo huo wa duka!! na mifano mingi tu ktk nafasi mbali mbali za kimaendeleo, sasa inabidi niwaamshe wagosi wenzangu waamke ili wakuze jiji lao na sio tukubali wageni watupige bao katika nyumba yetu KWA AMANI NA SIO VITA(muelewa ataelewa)

Sasa tazama mtoto wa kichaga manka anavyotisha barabara ya 20(bara 20 ndo' tunavyoita watoto wa tanga mfano- n'da bara 20 yani naenda barabara ya 20) manka anatusua ugenini,anapiga mzigo kwa kujituma masaa 10 au 12 na zaidi mtu yupo golini tu akitoka kamuachia mwingine aendelee, hamna kufunga duka hapo hadi jua lizame!! tazama maduka ya wachaga kule SAFI SANA WATU WANA MAKE MAISHA YAO!!

Sasa sisi watanga tumekosa nini hadi tuwe nyuma hivi!!?mgeni kamficha mzawa, na hili lipo mikoa mingi sana ila ni katika hali ya kuiamsha tanga...na kuwapa challenge wengine na sio kama nawachukia wachaga...maana ni ruhusa kuweka makazi popote na kufanya kazi!! ni sawa useme hawa yanga hawatuwezi jamani wapigeni bao, sio kama unawachukia yanga u knw it!!!

SO AMKENI TANGA IKIFIKA 2030 TUWE TUMEPIGA HATUA
SO WACHAGA KAZENI HIVO HIVO NA ZAIDI IKIFIKA 2030 TUWE TUPO KILELE CHA MBALI SANA
hip hop z all about movement, inspiration - positively!!!


Endelea kumfatilia Roma katika ukurasa wake wa facebook kwa ufafanuzi wa mashairi yake

0 comments:

Post a Comment