Jana jumatatu ilikua siku ya kuzaliwa ya Kanye West na alitimiza umri wa miaka 38.
Mke wake Kim Kardashian aliamua kumfanyia suprise kwa kumkodishia uwanja wa kikapu wa Staples Center uliopo Los Angeles kwa siku nzima ya jana ambao hutumika kwa ajili ya timu za mpira wa kikapu Marekani.
Baadhi ya watu wa karibu waliolikwa kwenye tafrija hiyo ni Justin Bieber, Tyga, Pusha Tna John Legend ambaye alikua MC wa shughuli hiyo.
Kim pia aliwalipa makocha wa Lakers kwa ajili ya kuchezesha mchezo huo pamoja na baadhi ya wasichana ambao waliongeza mvuto kwa kumshangilia mume wake muda wote.
0 comments:
Post a Comment