
Refa wa mechi za ligi kuu ya England Phil Dowd amejibu kwa vitendo
shutuma zilizoelekezwa kwake kwa uzito aliokuwa nao baada ya kurudi kwa
ajili ya msimu mpya akiwa amepungua uzito .
Dowd ambaye alikuwa na kitambi ambacho wakati mwingine kilikuwa
kinamfanya ashindwe kukimbia wakati wa mechi kubwa alijiandikisha kwenye
gym ambayo amekuwa akifanya mazoezi kwa miezi miwili ambapo amefanikiwa
kupungua uzito na kuonekana mwembamba .

Huu ndio muonekano mpya wa mwamuzi Phil Dowd baada ya miezi miwili ya mazoezi.
Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ambaye
amezoeleka kwa tabia yake ya kuwashutumu waamuzi pale ambapo timu yake
isipofanya vizuri alizungumzia suala la uzito wa refa Phil Dowd baada ya
mchezo baina ya Manchester United na Arsenal uliochezwa mwezi aprili
mwaka huu baada ya Refa huyo kuwaonyesha wachezaji watano wa United kadi
ya njano. Ferguson alisikika akisema kuwa ” refa huyu hakuweza kuendana
na kasi ya mchezo na alikuwa anatoa kadi kila anapoona tukio
limetokea”.

Cheki kitambi kilivokuwa kabla ya mazoezi .
Phil Dowd aliwahi kushindwa kufikia viwango stahiki vya afya kabla ya
msimu uliopita ambapo alilazimika kufanya mazoezi na kupunguza uzito
kala yakuruhusiwa kuamua mechi za Epl Na mara zote amekuwa akitukanwa na
mashabiki kwa jinsi muonekano wake ulivyo na alivyokuwa anapata tabu
kukimbizana na wachezaji huku akiwa anaonekana amechoka
0 comments:
Post a Comment