
Mtandao wa Standard Digital Entertainment umethibitisha kuwa staa huyo wa hit ya ‘Kesho’ anategemea kufanya show nyingine katika viwanja vya Carnivore (August 9) jijini Nairobi, na kesho yake (August 10) ataelekea Mombasa katika show nyingine itakayofanyika katika hoteli ya Whitesands, hizi zote zikiwa zimeandaliwa na The Courtyards.
Pia jana tuliripoti juu ya show anayotegemewa kutumbuiza jukwaa moja na wasanii wa kimataifa kutoka Nigeria Ice Prince na Davido itakayofanyika Nairobi (July 27).
Ukiachilia show hizo Platnumz akiwa kama Coca boy anategemewa kushiriki katika kampeni ya Coca cola kama tunavyojua yeye ni balozi , ambapo akishirikiana na Mr Falvour wa Nigeria wataurudia nyimbo za marehemu Brenda Fassie “Vulindlela” pamoja na ule wa 2 Face Idibia “African Queen”. Hivi ndivyo muziki unaweza kubadilisha maisha ya kijana wa kiTanzania endapo utauchukulia serious kama kazi, juhudi na uvumilivu ndio silaha ya vita hii. Big up Platnumz you deserve it man
0 comments:
Post a Comment