Saturday, June 8, 2013

Is it serious!? Salama Jabir asema huenda siku moja akaolewa na AY


AY na Salama



Mtangazaji mahili wa show za TV/Radio aliyeisimamisha wima show mpya na kali inayorushwa kupitia channel 5 ‘Mkasi’ namzungumzia Salama Jabir ametupia ‘neno’ kupitia kipindi hicho kuwa heunda siku moja akaolewa na AY!


Kama uliingalia show ya Mkasi jumatatu ama marudio yake leo (jumamosi) ambapo crew nzima ya kipindi cha mkasi chini ya C.E.O na Producer wa show Ambwene Yesaya ‘AY’ walikuwa wakieleza changamoto na mambo mbalimbali waliyokutana nayo wakati wanaanza kufanya kipindi hicho, mwishoni Salama ambae alikuwa akimuelezea AY kuwa ni msanii ambae anajivunia kufanya nae kazi kutokana na jinsi alivyomchapakazi na mtu wa kuaminika alimaliza kwa kusema “huenda ipo siku moja tutaona..!”.


Wote tunajua Salama alivyo mtu wa utani sana, kitu kinachoongeza burudani ya ziada katika show zake, alitamka hivyo na kumgeukia AY akimuuliza, na AY mwenyewe akajikuta anacheka na kukubali,of course it was just a joke a.k.a utani tu, lakini hakuna aijuae kesho ukizingatia wote wako single!


Show ya Mkasi ambayo imefanikiwa kuteka attention ya watazamaji wengi kutokana na ubora wa hali ya juu na jinsi ilivyo-well organized inaundwa na crew ya wataalam wa mambo mbalimbali ya media waliobobea, and that’s why it is among the best TV shows kwa Tanzania, na kwa zinazofanyika nje ya studio inaweza kushika namba moja ikiwa na idea mpya kabisa hapa kwetu japo huko mtoni zipo za hivo.
Sasa crew hiyo imeanza ku-shoot vipindi vipya kwa ajili ya show hiyo tayari kwa kuirudisha tena hewani ikiwa na ubora zaidi.


ikitokea kweli utani ukawa ukweli, AY na Salama hii couple itakuwaje?

0 comments:

Post a Comment