Sunday, June 9, 2013
Home »
» Kala Jeremiah, Ommy Dimpoz, Diamond na Chalz Baba waibuka na tuzo nyingi zaidi kwenye KTMA 2013 soma hapa na list nzima washindi hapa
Kala Jeremiah, Ommy Dimpoz, Diamond na Chalz Baba waibuka na tuzo nyingi zaidi kwenye KTMA 2013 soma hapa na list nzima washindi hapa
Rapper wa Mwanza, Kala Jeremiah amefanikiwa kuibuka na tuzo tatu ikiwemo kubwa ya wimbo bora wa mwaka kwa hit yake ‘Dear God’. Kala alishinda pia tuzo ya msanii bora wa Hip Hop kwa kuwabwaga Fid Q, Joh Makini, Profesa Jay na Stamina kwenye kipengele hicho.
Naye Ommy Dimpoz ameibuka na tuzo tatu zikiwemo za wimbo bora wa Bongo Pop na wimbo bora wa kushirikiana/Kushirikishwa kwa hit single yake Me and You. Pia hit yake Baadaye imechukua tuzo ya video bora ya mwaka.
Licha ya kutokuwepo wala kutuma mwakilishi, Diamond alifanikiwa kushinda tuzo kubwa ya pili kwa usiku huo ya msanii bora wa kiume kwa kuwabwaga Ben Pol, Linex, Mzee Yusuf na Ommy Dimpoz na pia kushinda tuzo ya Msanii bora wa kiume Bongo Flava.
Tuzo za muziki wa dance zilitawaliwa na Chalz Baba wa Mashujaa Band aliyeibuka tuzo mbili za Msanii bora wa kiume Bendi na Mtunzi bora wa mashairi – Bendi.
Usiku wa tuzo za KTMA ulipambwa na burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiwemo Linah, Amini, Richie Mavoko, Mataluma, Hussein Jumbe, Zahir Zorro, Patricia Hillary na Barnaba. Wengine ni Snura, Godzilla, Mabeste, Madee na Afande Sele.
Host wa tuzo hizo mwaka huu alikuwa ni Zembwele na TJ.
NA HII NDO LIST NZIMA YA WASHINDI
Wimbo bora wa mwaka-Kala Jeremiah ‘Dear God’
Msanii bora wa kiume-Diamond
Msanii bora wa kike-Lady Jay Dee
Msanii bora wa kike-Taarabu (Isha Mashauzi)
Msanii Bora wa kiume Taarabu-Mzee Yusuph
Msanii bora wa kiume Bongo fleva-Diamond
Msanii bora wa kike Bongo fleva-Recho
Msanii bora wa Hip Hop-Kala Jeremiah
Msanii bora wa kiume Band-Chalz Baba
Msanii wa bora wa kike Band-Luiza Mbutu
Msanii bora anaechipukia-Ali Nipishe
Video bora ya wimbo bora ya mwaka-Ommy Dimpoz ‘Baadae’
Mtunzi bora wa mashairi Taarabu-Thabeet Abdul
Mtunzi bora wa mashairi bongo fleva-Ben Paul
Mtunzi bora wa mashairi Hip Hop-Kala Jeremiah
Mtunzi bora wa mashairi Band-Charles Baba
Mtayarishaji bora wa mwaka Muziki wa kizazi kipya-Man Walter
Mtayarishaji wa wimbo wa mwaka Taarabu-Enriko
Mtayarishaji wa wimbo wa mwaka band-Amoroso
Mtayarishaji chipukizi wa mwaka-Mesen Selecta
Rappa bora wa Band-Fagasoni
Wimbo wenye vionjo vya asili-Mrisho Mpoto ‘Chocheeni Kuni’
Wimbo bora wa band-Mashujaa Band
Wimbo bora wa Reggae-Kilimanjaro ‘Warriors from the East’
Wimbo bora wa Afrika Mashariki- Jose Chameleone ‘Valu Valu’
Wimbo bora wa Bongo Pop-Ommy Dimpoz ft Vannessa ‘me and you’
Wimbo bora wa kushirikiana/Kushirikishwa- Ommy Dimpoz Feat.Vanessa Mdee ‘Me and U’
Wimbo bora wa Hip Hop-Nay wa Mitego ‘Nasema Nao’
Wimbo bora wa RnB- Kuwa na Subira ‘Rama Dee’
Wimbo bora wa Ragga/Dance hall-Dabo ‘Predator’
Wimbo bora wa Taarabu-Khadija Kopa ‘Mjini chuo Kikuu’
Wimbo bora wa Zouk/ Rhumba-Amini ‘Ni wewe’
Band Bora ya Mwaka-Mashujaa Band
Kikundi bora cha Taarab-Jahazi Modern Taarabu
Kikundi bora cha muziki wa kizazi kipya-Jambo Squad
*Hall of Fame-Kilimanjaro Band ‘Wana Njenje’
*Salum Abdallah Yazidu (aliyefariki mwaka 1965, alitamba na kibao chake shemeji shemeji)
0 comments:
Post a Comment