HAO NI BAADHI YA WANAZIKI WALIO CHUKUA HATUA |
Umoja
wa wanamuziki wa Bongo Flava, Rhumba, Dance, muziki wa Injili na aina
zingine leo umetoa agizo kwa makampuni yanayouza miito ya simu nchini
pamoja na makampuni ya simu kuiondoa miitio hiyo ndani ya siku saba
kuanzia leo
mpaka pale watakapokubaliana mikataba mipya.
Katika barua hiyo iliyoandikwa kwenda kwa waandishi wa
habari na iliyosainiwa na wasanii zaidi ya 150 nchini, wasanii hao wameyataka
makampuni ya simu kuondoa matangazo ya ringtone hizo kwenye radio, magazeti, tv,
website na kwenye ujumbe mfupi wa simu.
Hatua hiyo imechukuliwa na wasanii hao baada ya kubaini
kuwa makampuni ya simu yanawanyonya kwa kiasi kikubwa kwa kuwalipa chini ya
asilimia 10 ya mauzo ya ringtone hizo huku yenyewe yakibaki na zaidi ya asilimia
80.
Wiki iliyopita mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe aliliibua
suala hilo bungeni na kudai kuwa imeundwa kamati itakayoangalia upya utaratibu
wa mauzo ya ringtone.
Press Release ndio hii.
YAH: KUFUTA MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA
BONGO FLEVA,GOSPEL,DANSI NA TAARABU KWENYE MITANDAO YA SIMU.
Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Kwa ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya
muziki wa Gospel, Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agzio
kwenu la kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na
Callertunes katika mitandao ya simu ya Vodacom, Zantel,Tigo na Airtel na kufuta
mkataba tuliosaini kati yetu sisi Wasanii na Kampuni yako mpaka hapo
tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa muziki wetu, pamoja
na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna mpya ya sisi na nyinyi tutakavyofanya
kazi.
Sababu ya sisi Wasanii kusimamisha na kufuta mikataba
kati yetu na wanaofanya biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika
kushindwa kuweka wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda
husika kama ilivyoanishwa katika mikataba husika.
Sababu ya pili ni mitandao ya simu kuchukua kiasi
kikubwa cha fedha ambacho ni asilimia themanini ya mauzo yote ya maudhui yetu,
jambo hili linatuumiza na limetufanya tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja
ya pato toka kwenye shoo.
Hivyo tumeziagiza kampuni zote zinazofanya kazi ya kuuza
maudhui yetu kutoa maelekezo kwenye mtandao husika kuwaelekeza kusimamisha
mauzo ya kazi zetu za sanaa ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 30/07/12
ikiwa pamoja na kusimamisha matangazo yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu kwa
njia ya Television , Radio , blogs, website, Magazeti na Ujumbe Mfupi wa maneno
mpaka hapo tutakapofikia muafaka.
Jumla ya wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine
wanaendelea kusaini.
Mwisho tunawashukuru kwa ushirikianao wenu, na
tunaambatanisha sahihi zetu ili kuonyesha uthibitisho wa umoja wetu katika
jambo hili.
Asante.
0 comments:
Post a Comment