Chelsea wanaongoza ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama 56,Totenham wako nafasi ya pili wakilingana pointi na Arsenal walioko nafasi ya tatu wakiwa wote na pointi 47.Liverpool wako nafasi ya 4 na alama 46 sawa na Man City nafasi ya 5 na alama 46 huku Manchester United wakiwa nafasi yao ya 6 na alama zao 42.
Lakini mshambuliaji wa Chelsea hawaogopi Tottenham wala Liverpool wala Man City.Eden Hazard anawaogopa sana Manchester United na Arsenal anaziona ndio timu tishio katika safari ya ubingwa.Hazard anawaona United walioko nafasi ya 6 wanaweza kuchupa hadi kuwakaribia kwani tofauti kati ya United na Tottenham ni alama tano tuu.
Kauli hii inakuja siku chache kabla ya Chelsea kuwakabili Arsenal,”United walifanya vibaya raundi ya kwanza lakini siku za usoni wanacheza vizuri sana,wana kocha mzuri na timu yao ni bora sana nadhani wanakuja kwa spidi kubwa sana” aliongea Hazard wakati wa mahojiano na Thiery Henru ambae ni mchambuzi wa soka katika kituo cha Sky Sports.
“Tottenham ni wazuri sana lakini kwangu uzoefu wa Manchester United naona unaweza kuwafanya tuwahofie kwa sasa”,aliongeza Hazard.Hazard anaamini uzoefu wa United na Arsenal unaweza kuwa hatari zaidi kwao katika kipindi hiki cha mwisho cha kuusaka ubingwa.
Kuhusu makocha wawili Conte na Mourinho.Hazard anaamini Conte ana mbinu sana kwani muda mwingi mazoezini amekuwa akiwapa mazoezi ya kimbinu zaidi tofauti na Mourinho ambae hawakuwa wanafanya vitu vingi ila alikuwa akiwaamini wachezaji wake kwa kuwa wanajua cha kufanya.Hazard anasema kwa sasa anafurahia mbinu za Conte kwa kuwa anampa sana nafasi kushambulia.
0 comments:
Post a Comment