Monday, July 29, 2013

Maajabu: Mtoto wa kike aliyezaliwa bila fuvu Nigeria kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwekewa fuvu la kutengeneza

Wazazi wa mtoto wa kike nchini Nigeria aliyezaliwa na kugundulika hana fuvu, wanategemea ‘miujiza’ ya uponyaji katika upasuaji mkubwa wa kuokoa maisha ya mtoto huyo anayetegemea kuwekewa fuvu la kutengeneza.
nigeria mtoto-2
Okikijesu Olawuyi aliyezaliwa May 11, 2010 aligundulika kuwa na tatizo ambalo halijawahi kuingia katika rekodi ya dunia kwa kukutwa asilimia 50 ya fuvu lake haipo.
Madaktari bingwa wa daraja la kwanza kutoka hospitali ya John Hopkins ya Marekani wanaopigania uhai wa binti huyo wanategemewa kumfanyia upasuaji wa kutengenezea fuvu kwa kutumia mifupa ya mikono yake itakayosaidia kutengeneza mfupa utakaomsaidia kuendelea kuishi kama zoezi hilo litafanikiwa, Naija gists iliripoti.
Wataalam hao wameitaja hali hiyo kuwa ni ‘Congenital Cranial Deficiency’.
Wachambuzi wanasema hili litakuwa ndio tukio la kwanza la aina hiyo kuonekana duniani kwa mtoto kuzaliwa akiwa hana fuvu huku madaktari wakiongeza kuwa haijawahi kutokea tatizo kama hilo katika historia ya matibabu duniani hivyo hili ni tukio la kipekee kuwahi kutokea.
Wazazi wa mtoto huyo wana imani na madaktari watatu bingwa wanaomshughulikia mwanao japo kikwazo kikubwa wanachokutana nacho ni gharama kubwa sana zinazohitajika kukamilisha zoezi la kuokoa maisha ya mtoto wao.
Kwa mujibu wa wataalam wanasema kama zoezi hili litafanikiwa hili litakuwa moja kati ya maajabu yanayostahili kuingia katika kitabu cha rekodi za maajabu ya dunia ‘Guinness Worl book of records’.

0 comments:

Post a Comment