Kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanywa na chuo kikuu cha Bristol cha nchini Uingereza, watu wanaosoma habari mtandaoni (website/blogs) hupenda kusoma mambo mapya kuhusu mastaa ama maceleb au kuhusu masuala ya mitindo. Umegundua kuwa wasomaji hawavutiwi ‘kabisa’ kusoma habari kuhusu siasa ama uchumi.
Wasomaji wa habari za mtandaoni huvutiwa zaidi kufahamu mambo kuhusu watu maarufu (kwa Tanzania mfano Diamond ama Wema Sepetu) kuliko masuala mengine hata kama ni ya muhimu katika maisha yao.
Watafiti hao walitumia website ya nchini Australia, News.com.au walibaini kuwa zile zilizokuwa na maneno kama ‘woman’, ‘sex’, ‘girl’, ‘porn’ na ‘mum’ zilikuwa maarufu zaidi.
Kwa wasomaji wa website ya Forbes, habari zenye maneno kama ‘richest’, ‘app’, ‘best’ na ‘worst’ ziliwavutia zaidi.
Lakini habari zilizokuwa na maneno kama share’, ‘stock’ ama ‘dividend’ hazikuwa na umaarufu.
Timu hiyo ilichunguza website tofauti 14 katika kipindi cha miezi 18. source bongo 5
0 comments:
Post a Comment