Monday, June 24, 2013

Picha jinsi mtaa wa 'Ngono' ulivyo fumuliwa ANGALIA HAPA JINSI ILLIVYO KUWA



NI hakika ‘mtaa wa ngono’ umefumuliwa! Sakata hilo lilijiri saa tisa usiku, Ijumaa iliyopita, Barabara ya Shekilango, kuanzia Bamaga hadi Sinza Mori jijini Dar eneo ambalo makahaba wameligeuza chumbani.

Kwa mujibu wa takwimu za kiserikali, eneo hilo (kuanzia Bamaga hadi Sinza Mori) limekubuhu kwa wasichana kujiuza nyakati za usiku huku makao yao makuu yakiwa eneo la Afrika Sana hasa pembezoni mwa Corner Bar. Mmoja wa viongozi wa serikali ya mtaa ya eneo hilo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alisema.

“Tumejitahidi sana kushirikiana na polisi ili kutokomeza ukahaba eneo hilo lakini wapi! Hawa mabinti ni wabishi, mbaya zaidi wamelifanya eneo hili kuwa la ngono. “Watoto wetu wanapita usiku pale wanawaona wanavyofanya, wanatuharibia kizazi kijacho, kama wao wamejishindwa wasiwaambukize wengine.”

Siku ya tukio, saa tisa usiku, askari wa ulinzi shirikishi walijipanga kwa ajili ya kuufumua mtaa huo huku wakiwa na tahadhari kufuatia habari za kiintelijensia kudai kuwa, makahaba hao walipanga kuua mtu punde watakapovamiwa. Askari hao wakiwa kwenye doria ya kila usiku, waliwavamia makahaba hao eneo lenye majani madogo katikati ya Afrika Sana na Mapambano upande wa yadi ya Mwanamboka wakiwa na wateja wao wakifanya ngono hadharani.

Katika hali iliyoonesha makahaba wamejiimarisha kwa ulinzi siku hizi, wakati wa zoezi hilo, machangu hao sanjari na vibaka wanaowaunga mkono wakisemekana ni ‘walinzi’ wao, waliokota mawe na kuwarushia askari hao hali iliyozua tafrani zaidi

Ndipo piga nikupige ilipozuka ambapo askari walionesha umahiri wao wa kupambana na wahalifu kwa kuwadhibiti kwa vichapo vya hapa na pale na kufanikiwa kuwaweka wengi chini ya ulinzi. Kuona hivyo, baadhi ya makahaba na wateja wao walifanikiwa kuwachoropoka askari bila nguo na kutokomea gizani hivyo kulifanya eneo hilo kuwa jeupe.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya makahaba waliokimbia walijikuta wakiacha kwenye majani nguo zao za ndani na kuzua maswali kwamba ni kwa nini hawakuwa wamezivaa!
“Jamani hizi si nguo zao za ndani? Iource Global Publishe

0 comments:

Post a Comment