Vyanzo vilivyo karibu na KK vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Kim alijifungua salama kwa njia ya kawaida (Natural child birth) na huku akiwa amewahi kwa wiki 5 kabla ya tarehe iliyokuwa inategemewa.
Vyanzo hivyo vinasema Kim alianza kupata dalili Ijumaa usiku (June 14) na siku iliyofuatia Jumamosi asubuhi alipelekwa katika hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center huko Beverly Hills,na kupelekwa moja kwa moja sehemu ya kujifungulia, na akajifungua jana Jumamosi (June 15).
Hili ndio jengo la hospitali ya Cedar alipojifungulia Kim K
Cedar ni hospitali ambayo mastaa wengi wamejifungulia watoto wao akiwemo Britney Spears, Jessica Simpson, Victoria Beckham na wengine.
Baba wa mtoto Kanye West hakuwa mbali na mpenzi wake toka wanafika hospitali mpaka katika chumba cha kujifungulia alikuwepo pembeni ya KK huku akishuhudia zoezi zima la la mwanao akianza kuvuta hewa ya duniani.
Vyanzo hivyo vimeendelea kusema Kanye West aliahirisha kuhudhuria party ya kuachia wimbo wake mpya Ijumaa usiku(June 14) mara tu baada ya Kim kumwambia hajisikii vizuri na kuongozana na mpenzi wake mpaka hospitali.
Kim K na mwanae ambaye bado hatujajua atapewa jina gani wako na afya njema kabisa, vyanzo vimethibitisha.
Huyu ndie mtoto wa kwanza wa mastaa Kanye West na Kim Kardashian
0 comments:
Post a Comment