Usimchukulie poa anaekupigia makofi wakati unacheza, huwezi jua na yeye pia anaweza kuwa mchezaji tena zaidi yako, ila inahitaji busara ya ziada kumuuliza anaekupigia makofi akupe style anayopenda uicheze ili aendelee kukupigia makofi zaidi!?Sawasawa...Kala Jeremiah ameweza hii..
Mshindi huyo wa tuzo tatu za Kili, aliyetisha sana na vina vya ‘NE’ kwenye wimbo wake wa Dear God sasa anaendeleza mashambulizi na amehamia kwenye vina vya ‘MBA’ ambapo ameamua kuwashirikisha fans wake wa facebook ili kukamilisha uandishi wa ngoma hiyo.
Kala alipost kwenye ukurasa wake wa facebook kipande cha mashairi ya wimbo kisha akawaambia fans wamalizie.
Leotainmenttz ilipiga story na Kala kutaka kujua kulikoni mashairi yale mazuri aliamua kuyamwaga facebook?
“Unajua mimi siku zote napenda sana kuwa connected na mashabiki wangu, kwa hiyo unajua vitu kama hivyo nafanya kuwaweka karibu na mimi lakini pia kushiriki nao vitu, kama kwenye album yangu ya Pasaka kuna remix ya ‘Dear God’ nilifanya na mashabiki , kupitia page yangu nilipata mashabiki ambao walichana mle, kwa hiyo sometimes huwa najaribu kuangalia humuhumu kuna vipaji pia, kama ukiangalia hizo comments kuna watu wameandika mashairi mazuri, wameandika vitu vizuri vinavyoweza kufanya kitu.”Alifunguka Kala.
Leotainment ilitaka kujua kama mkali huyo anaweza kuufanya wimbo huo kuwa official realease baada ya mashairi kukamilika, “Yeah, kabisa, kabisa kabisaa….,”Alisisitiza Kala Jeremiah
So kama we ni fan wake na unakipaji changia mashairi uwe pround kushiriki kwenye kitu kizuri toka kwa msanii unayempenda.
Hiki ndicho kipande cha verse alichoweka Kala kwenye ukurasa wake wa facebook June 27, na fans wake kibao walichangia mistari:
“iNAANZA DINGI ANANIAMBIA NIHAME HOME NIKAPANGE CHUMBA
NAMPIGIA SIMU MCHUMBA
NAMWAMBIA NITAFUTIE DALALI ILI ANITAFUTIE NYUMBA
ANASHTUKA heee! akutafutie nyumba?
NAMJIBU YES DINGI NYUMBANI AMEZIDI KUGOMBA
NAKATA SIMU NAJISACHI MFUKONI SINA MAVUMBA
NAPANDA DALADALA KUELEKEA KWA WANANGU WAUZA MTUMBA
ILE NAFIKA TU KABLA SIJAAELEZA YALIYONIKUMBA
MARA MGAMBO WA JIJI............................................................
jaza maneno hapa kukaamilishaa mstaari huu. hahahahahahaha TWENDE...”!
0 comments:
Post a Comment