Ni
wiki kadhaa tu zimepita ambapo Nice Lucas Mkenda aka Mr. Nice alirudi
kwa kishindo kwenye vyombo vya habari. Baada ya kusaini mkataba mnono na
GrandPa Records ya Kenya, Nice aligeuka kama mfalme.
Kwa muda mfupi alifanikiwa kufanya interview kwenye radio na TV zote
kubwa za Kenya. Nice alitawala headlines za magazeti na hata blogs za
burudani kutokana na watu kuamini kuwa huo ni ujio mpya na wa kishindo
wa msanii huyo aliyekuwa amepotea kabisa.
GrandPa Records waliita wana habari waliomuuliza maswali kwa shauku
Mr. Nice ambaye aliyajibu kwa ufasaha na ustadi mkubwa. Kwenye interview
za TV na radio, Nice aliongea kwa mamlaka na kujiamini, kitu
kilichotupa ishara kuwa, msanii huyu aliyekuwa na sifa mbaya za ulevi
amebadilika kabisa na kwamba hii ndio nafasi yake ya pili kurekebisha
makosa yake na kurudi tena kileleni.
Kumbe tulikosea. Nice alikuwa amebadilika kwa nje tu lakini ndani
alikuwa ni yule yule. Maisha magumu na kusota mtaani havijambadilisha
chochote. Kwa muda mfupi tu tangu achukuliwe na label hiyo, Nice alitoa
makucha yake na kugeuka kuwa mzigo.
Inadaiwa kuwa Nice alianza kuwakera GrandaPA kwa tabia yake ya ulevi,
kushindwa kwendana na ratiba ya studio na kuonesha picha mbaya kwa
label hiyo. Kwa mujibu wa Pulse
ya Standard Media, Kenya, Mr Nice aliwahi kupigana na dereva aliyekuwa
akimwendesha, Oro kwenye studio. Pia alikuwa na tabia ya kuingiza
wanawake na kulewa studio.
CEO wa Grandpa, Refigah aliiambia Pulse kuwa kuna siku Nice alilewa
hadi kushindwa kulipa bili hali iliyomlazimu promoter aitwaye Dickson
kumuokoa. Aliongeza kuwa nusu ya pesa aliyokuwa akiipata ilikuwa ikiisha
kwa kuinywea pombe ama kula bata na wanawake.
Refigah alidai kuwa kuna wakati Nice alikuwa akilewa hadi kuanza
kuwachezea na kuwasumbua wanawake studio. Kulikuwa na ratiba afanye
collabo na Ragga D na Nameless lakini ilishindikana kutokana na tabia
yake mbaya.
Siku moja kabla ya kuitisha waandishi wa habari kutangaza uamuzi wa
kumpiga chini, label hiyo ilikuwa busy kumnyang’anya kila kitu
walichokuwa wamempa. Walienda kwenye nyumba waliyokuwa wamempatia jijini
Nairobi na kuchukua furniture zote walizokuwa wamemwekea mbele ya
mashahidi na polisi.
Tunasubiri kusikia upande wa pili wa story hii kutoka kwa Nice
mwenyewe lakini kama ndivyo alivyofanya basi amezingua mbayaaaaa!!
Friday, June 7, 2013
Home »
» Details: Ulevi, uzinzi na starehe vimemponza Mr.Nice
0 comments:
Post a Comment