Sheria ni msumeno na ikikata inakata kote, lakini pia sheria inayotumika kushitaki inaweza kumpa mshitakiwa haki ya kuendelea kufanya alichotuhumiwa endapo itakapobainika kuwa ilikuwa ni haki yake, wenyewe wanasema ‘ujue kucheza na vifungu’.
Mkali wa kuimba na kuvunja Chis Brown amegomea amri ya polisi wa jiji la Los Angeles iliyoambatana na barua maalum ya uongozi wa jiji ikimtaka kufuta machata ya kutisha aliyochora kwenye nyumba yake na kufuatia malalamiko yaliyotolewa na jirani zake kuwa yanawatisha watoto wao.
Kwa mujibu wa gazeti la Los Angeles Times, Chris Breezy amekata rufaa na kwa kutumia kifungu cha sheria za U.S.A kinachoeelezea uhuru wa kujieleza (freedom of expression). Mwimbaji huyo amemtumia mwanasheria wake Mark Geragos kuiandika kisheria rufaa hiyo.
Katika utetezi wa Breezy, michoro hiyo ni kazi ya sanaa inayolenga kupendezesha nyumba yake binafsi na kwamba haihusiani na matangazo kwa hiyo haiitaji kupata kibali chochote.
Rufaa hiyo imesisitiza kuwa uchoraji wa machata hayo ni sehemu inayoonesha kazi ya sanaa ya mmiliki wa nyumba hiyo na kwamba inaakisi uhuru wa kujieleza unaolindwa na sheria ya nchi hiyo(1st Amendment).
Michoro ya machatta hayo yalionesha kipaji kingine alichonacho Chris Brown, na kwa kuwa ndo kwanza anaanza kukifanyia kazi huenda akachora machatta mengine zaidi kama atashinda katika rufaa yake.
Mwimbaji huyo aliwashangaa majirani zake na kuwaona kama wanamfatilia sana kwa kuwa movie inayoangaliwa sana na watoto ya Harry Potter inaviumbe wengi wa kutisha kuliko hayo machata yake.
0 comments:
Post a Comment