Kuwa
na ‘unique identity’ ni moja ya technics nzuri kibiashara kwa msanii
sababu inafanya atambulike kirahisi na kwa haraka miongoni mwa wasanii
wengi.
Hakuna ubishi kuwa baba kijacho Nay Wa Mitego is running the game right now, kupitia hit song aliyoshirikiana Diamond Platnumz.
Nay amekuja na style yake ya kuvaa viatu viwili vya pair mbili
tofauti na ndivyo anavyoonekana mara zote anapokuwa popote iwe ni kwenye
show au mtaani. Kama bado unashangaa au hujaelewa ni hivi, mfano
anakuwa na pair mbili za viatu lets use Adidas na Puma, pair moja iwe
nyeupe na nyingine nyeusi, mguu mmoja anavaa Adidas nyeupe na mguu
mwingine anavaa puma nyeusi, that’s his new swag, sio uchawi lakini!!
Akiielezea style yake hiyo ya uvaaji viatu kupitia kipindi cha Hot
Mix cha EATV Nay amesema “navaa hivi nikimaanisha binadamu hatufanani,
wewe huwezi kuwa sawa na yule na mi siwezi kuwa sawa na wewe that’s the
big point”.
Wapo wasanii wengine wa nje na hapa Tanzania ambao wamewahi kujaribu
kufanya vitu vya kuwatofautisha na wengine. Mfano kwa nje kundi la Kriss
Kross wao style yao ilikuwa ni kugeuza jeans mbele kuwa nyuma na nyuma
kuwa mbele.
Hapa Tanzania mwana mashairi Mrisho Mpoto ana aina yake ya mavazi
anayovaa muda mwingi yanayomtambulisha na pia mara kadhaa huwa anatembea
peku bila viatu
0 comments:
Post a Comment