Tamaa ya kutaka kurekebisha viungo na muonekano aliokupa Mwenyezi Mungu eti ili ufanane na flani inaweza kugeuka kuwa zaidi ya hatari kama iliyomkuta mama huyu aliyefahamika kwa jina la Apryl Michelle Brown mwenye umri wa miaka 46 ambaye ndoto yake ilikuwa kuwa na muonekano kama wa Jennifer Lopez ama Janeth Jackson na badala yake akajikuta kapoteza mikono, miguu na sehemu ya makalio yake.
Mama huyo mkazi wa Los Angeles Marekani alikua ni mfanya kazi wa saloon ya kike kwa muda mrefu lakini maelezo ya mtaani na kutamani kubadili umbo lake vilimponza na baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu tangu alipoteza viungo vyake vya mwili aliamua kujitokeza hadharani kueleza ili kuwanusuru watu wengine.
Apryl ambae pia ni mama wa watoto wawili alisema, “nahitaji kushare story yangu kwa watu wengine ili kutoa onyo hasa kwa upasuaji na matibabu ya haraka na haramu, mimi sikujua hatari yake, nilidhani ni sindano isiyo na madhara ambayo ingenipa makalio niliyoyahitaji, kumbe haikuwa salama kwa matumizi ya binadamu, baada ya kutumia mwili wangu ulipata madhara makubwa almanusura nipoteze maisha, niliteseka nikafikia point nikaona kifo kingenipumzisha, lakini njia pekee ambayo Daktari angeweza kuyanusuru maisha yangu ilikuwa ni kuniondoa sehemu ya makalio, kunikata miguu yote na mikono.”
Mama huyo aliyesimulia mkasa wake kwa masikitiko makubwa alijilaumu na kujutia kwa kuwa alitumia pesa nyingi kukamilisha zoezi la kuchoma sindano kwa watu wa mtaani wanaofahamika kwa jina la “Pampers” ambao hujiita madaktari wakiwa mtaani na kutoa huduma kwa bei nafuu.
Alisema aliona rafiki zake wakiwa wamefanya zoezi hilo na akaamini wamefanikiwa ndipo na yeye akaamua kuchukua uamuzi ambao mwisho wa siku uliyabadilisha kabisa maisha yake

0 comments:
Post a Comment