Mchoro huo uliochorwa na mchoraji maarufu raia wa Sweden Johan Andersson unatarajiwa kupigwa mnada na unakadiriwa kuingiza takribani $22, 000 na kwamba kiasi hicho chote kitapelekwa kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali yanayoendesha kampeni ya kurudisha amani nchini Congo.
Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 37 aliyatembelea makambi ya wakimbizi DR Congo na Burundi akiwa kama muwakilishi wa shirika la wakimbizi duniani UNHCR. Nia yake ya dhati ya kusaidia kurudisha amani chini Congo ni sababu iliyomfanya abariki zoezi la kupigwa mnada mchoro huo.
Mchoraji Andersson amesema story ya maisha ya Angelina imemgusa zaidi kwa sababu yeye pia alimpoteza mama yake kwa ugonjwa wa kansa ya matiti.
“Mama yangu alikuwa na ugonjwa mbaya wa kansa ya matiti nilipokuwa na miaka 15, wazo la kuondoa matiti yote kwa kweli liliniogopesha na alikuwa na bahati sana ya kufanyiwa upasuaji wa kawaida bila kuondolewa matiti yote. Story ya Angelina imenisukuma kuchora mchoro huu unaoonesha picha halisi.” Alifunguka msanii huyo.
Inasemekana Angelina Jolie amepanga kufanya upasuaji mwingine kuondoa kizazi kwa kuwa ameonekana kuwa na asilimia 50 ya kupata kansa baada ya kuondoa matiti yake yote alipogundua ana asilimia 87 ya kupata ugonjwa ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa jarida la People, muigizaji huyo anaweza kufanya upasuaji kabla hajafikisha miaka 40, na baada ya upasuaji huo hatoeweza tena kuzaa.
0 comments:
Post a Comment