Ikiwa
ni wiki chache zimebaki kabla ya miezi 9 ya ujauzito wa mpenzi wa Kanye
West, Kim Kardashian kutimia, hatimaye jinsia ya mtoto mtarajiwa wa
wapenzi hao mastaa imefahamika.
Jana (May 23) ilikuwa ni siku muhimu kwa wazazi watarajiwa Kim
kardashian na Kanye West kukutana na daktari kwaajili ya kupigwa
ultrasound kujua maendeleo ya kiumbe cha Kanye kilichoko ndani ya tumbo
la Kim, pia kuweza kufahamu jinsia ya mtoto wao mtarajiwa.
Kutokana na umuhimu wa appointment ya kujua jinsia ya mtoto mara
nyingi wazazi wote wawili huwa wanakwenda pamoja lakini Kanye hakuweza
kuungana na kipenzi chake kumuona daktari kutokana na kuwa na ratiba
ngumu, japo aliwahi kumwambia mpenzi wake huyo kuwa hatapenda kushiriki
katika reality show yao ya ‘The Kardashian’s’, ambayo ilikuwa
ikirekodiwa wakiwa hapo kwa daktari. Kim K alisindikizwa na wanafamilia
wake wakiongozwa na mama yake mzazi pamoja na dada zake wawili.
Baada ya Ultra Sound daktari alimwambia Kim K jinsia ya mwanae lakini
sehemu hiyo ilikatwa katika video clip ya reality show hiyo, hali
ambayo imefanya baadhi ya watu kuamini kuwa Kim na Kanye wamependa
jinsia ya mtoto wa iwe surprise kwa wengine japo habari za chini ya
kapeti zinasema wanatarajia kupata mtoto wa kike.
Kuashiria siku ya kujifungua imekaribia Kim K anategemea kufanya baby shower June 2 na kadi za mwaliko zimeshaanza kusambazwa. Mhariri wa Bongo5 yuko busy kufuatilia uwezekano wa kuhudhuria baby shower hiyo, just kidding!
Friday, May 24, 2013
Home »
» Jinsia ya mtoto mtarajiwa wa Kim K na Kanye West yafahamika, bashiri, a boy or a girl?
0 comments:
Post a Comment