Home
Friday, May 24, 2013
Home
» » HABARI YA KIONGOZI MWINGINE ZANZIBAR ALIYEMWAGIWA TINDIKALI SOMA HABARI KAMILI HAPA
HABARI YA KIONGOZI MWINGINE ZANZIBAR ALIYEMWAGIWA TINDIKALI SOMA HABARI KAMILI HAPA
By
GAX blog
11:59 AM
No comments
Wimbi la viongozi wa Serikali, dini, wanasiasa na wafanyabiashara kuhujumiwa kwa ikiwamo kumwagiwa tindikali limeendelea kujitokeza Zanzibar, baada ya Sheha wa Shehia ya Tomondo, Muhamed Said ‘Kidevu; kumwagiwa tindikali nyumbani kwake mtaa wa Tomondo mjini Zanzibar.
Tukio hilo limetanguliwa na kumwagiwa tindikali Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga, aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya mji wa Zanzibar Rashid Juma, na wamiliki watatu wa maduka ya pombe wenye asili ya Kiasia na mmoja alifariki dunia.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis, alisema kwamba Sheha huyo alimwagiwa tindikali juzi usiku majira ya saa mbili za usiku, na Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka na mtu aliyehusika na shambulio hilo.
Alisema kwamba Polisi baada ya kufika katika eneo la tukio walifanikiwa kuokota kopo lililokuwa na maji maji yanayosemakana kuwa tindikali na litatumika kwa shughuli za uchunguzi ikiwamo vipimo vya vidole na vipimo vyingine kwa kutumia mashine maalum ya vinasaba (DNA).
“Tumepata kikopo katika eneo la tukio, tutaangalia finger print na DNA pamoja na kutafuta walioshuhudia tukio hilo, matukio haya yanajirudia mara kwa mara, yanaweza kukomeshwa endapo wananchi watatoa ushirikiano kwa kuwataja wahusika” alisema Kamanda Mkadam.
Sheha huyo ambaye alilazwa katika hospitali ya Mnazi mmoja na kupatiwa matibabu chini ya ulinzi wa polisi, alisema baada ya kutoka msikitini alikwenda kununua chakula na kupeleka nyumbani kwake, lakini kabla ya kula chakula hicho aliamua kwenda kuchota maji nje ya nyumba yake.
Alisema akiwa amebeba ndoo mbili za maji, ghafla alikutana uso kwa uso na mtu aliyekuwa ameshika kitu mkononi na kumwagia sehemu za kichwani, usoni na kifuani na kukimbia.
“Nilipotoka kuchota maji, nilikutana na jamaa amebeba kikopo, mrefu, mweusi na amevaa ninja (mavin guy), akanimwagia kitu kama maji maji, baadae nikayahisi kuwa ni ya moto, nikapiga kelele, akakimbia na kutupa kikopo na kuanza kumfukuza, lakini nilishindwa kuendelea kutokana na maumivu makali," alisema Sheha Mohamed.
Alisema ana wasiwasi kuwa chanzo cha kumwagiwa kwake tindikali, ni kitendo chake cha kuwasindikiza Polisi katika eneo moja la mtaa wake, kuteremsha bendera mbili za Jumuiya ya Uamsho na mihadhara ya Kiislamu Zanzibar(Jumiki).
“Kwa hali hii tunayokwenda nayo Zanzibar, watatumaliza, matumizi ya tindikali yamekuwa silaha za maangamizi, tindikali imekuwa na nguvu kuliko hata silaha za moto,” alisema Sheha huyo na kuongeza.
“Kazi zetu ni za visasi, kutishiwa na kumwagiwa tindikali ni jambo la kawaida, ila ujumbe wangu kwa Watanzania siasa itatufikisha pabaya.”
Kwa upande wake, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alisema Serikali itatumia nguvu zake kuwasaka watu waliohusika na shambulio hilo na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
← Newer Post
Older Post →
Home
0 comments:
Post a Comment
Social Profiles
Popular
Tags
Blog Archives
American Music Awards 2013: Rihanna, Justin Timberlake ni miongoni mwa walioondoka na tuzo jana (Orodha kamili/Picha)
Jana Jumapili (Nov 24) limefanyika tukio la ugawaji wa tuzo za ‘American Music Awards 2013’ katika ukumbi wa Nokia Theatre L.A. Marek...
TAYGA NA MOVIE YA ROCK CITY XXX
TYGA Rapper wa Young Money, Tyga ameamua kuingia kwenye biashara ya movie za ngono kwa kuanzisha website yake mambo h...
New Song: Yaki ft. Nician "YULE" sikiliza na kudownload
Sikiliza hapa wimbo mpya wa Yaki "YULE"
CHEKI VIATU VIPYA AMBAYO LIL WAYNE AMEZINDUA - 'SPECTRE' AMBAYO IPO CHINI YA BRAND YA SUPRA
Hivi ndivyo party la uzinduzi wa Spectre za Lil Wayne ulivyo-go down Jumatano hii.
Kala Jeremiah, Ommy Dimpoz, Diamond na Chalz Baba waibuka na tuzo nyingi zaidi kwenye KTMA 2013 soma hapa na list nzima washindi hapa
Rapper wa Mwanza, Kala Jeremiah amefanikiwa kuibuka na tuzo tatu ikiwemo kubwa ya wimbo bora wa mwaka kwa hit yake ‘Dear God’. Kala alishi...
MUZIKI | DARKMASTER - TUSOMANE(Audio | Download)
Hii hapa ile Ngoma ambayo tuliisubiri kwa hamu ya kwake Mwanachemba DARK MASTER - TUSOMANE. Isikilize na Download hapa
NYIMBO YA BEN POL NA LINA --YATAKWISHA
BEN POL NA LINAH Idownload hapa audio music yakwake Ben Pol akiwa amemshirikisha Linah. Track inakwenda kwa jina la Yatakwisha.
Amazon - Mamito. (Official Video)
New Audio Song | Chikwaso ft Stamina & Deddy - MCHAKA MCHAKA
LIPUMBA awashangaa wanaostahili jela kuchukua fomu za Urais na Muhimbili yakaukiwa damu..#MAGAZETINI JUNE 15
MWANANCHI Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amechukua fomu ya kugombea urais kupiti...
G newz fan page
Search This Blog
Popular Posts
Kuhusiana na kesi ya Agnes Masogange, Soma hapa ujuwe mapya yaliyo ibuka
WAJANJA WAUGEUZA MSIBA WA NGWEA DILI, HIKI NDO WANACHOKIFANYA
Cheche za Feza Kessy zaanza kuonekana katika jumba la Big Brother, apata bahati ya kuwa mkuu wa nyumba
TAYGA NA MOVIE YA ROCK CITY XXX
Followers
About Me
GAX blog
MOROGORO, Tanzania
+255 759317968
View my complete profile
Networked Blog
Follow this blog
Categories
audio
magazine
NEWAS
PICHA
Sport
STORY
VIDEO
vidio
0 comments:
Post a Comment