Tuesday, May 28, 2013

Chris Brown kunusurika kwenda jela! Tuhuma zinazomkabili kukimbia msala baada ya kugonga gari zakanushwa




Mwimbaji wa ‘Fine china’ Chris Brown anaweza kuwa amenusurika kwenda jela hivi karibuni baada ya ripoti za awali zilizotolewa kuwa mwimbaji huyo alikwepa msala kijanjajanja baada ya kuligonga gari la mama mmoja aina ya Mercedez nyeusi wakati walipokuwa wakipiga misele na Karrueche Tran katika barabara za Los Angeles kukanushwa.


Ripoti hizo za awali zinamtuhumu mwimbaji huyo kwa kuficha baadhi ya vielelezo na taarifa ambazo zingemsaidia mmiliki wa gari waliloligonga kupata msaada wa kisheria na kulitatua tatizo kirahisi, ilisemekana kuwa Breezy alificha namba ya leseni yake ya udereva na baadhi ya vielelezo vya Bima.

Lakini chanzo cha kuaminika kimeiambia TMZ kuwa Chris alimpa mwanamke huyo taarifa zote alizozihitaji tofauti na tuhuma zinazoelekezwa kwake, pia mwanamke huyo alikata simu alipopigiwa na mwanasheria wa Chris Breezy, na picha za gari la mama huyo zilizochukuliwa wakati wa tukio zilionesha hakuna uharibifu uliojitokeza. Hadi sasa kitengo cha Polisi cha Los Angeles bado hakijamtafuta Chris kuhusiana na tukio hilo.


Wiki iliyopita Chris Breezy na Karrueche Tran walinaswa na Camera za paparazzi wakiwa nje ya gari lao kwa lengo la kuzungumza na mama huyo baada ya gari lao aina ya Range Rover kugonga Mercedez ya mama huyo.

0 comments:

Post a Comment