Adam Juma
Nisher kutoka A City ni mtayarishaji mpya wa video Tanzania ambae nyota yake 'njema' ilianza kuonekana asubuhi mwaka jana (2012) baada ya kipindi kirefu kupita bila kuwa na ushindani mkubwa wa kiuwezo katika utayarishaji wa videos bongo. Katika kile kinacho prove nyota yake njema imeanza kuonekana ni pale director anaeaminika kukosa mpinzani kwa muda mrefu Adam Juma wa Visual Lab alipotamka kitu kuhusu kazi za Nisher wiki moja iliyoipita.
Nisher
Kupitia akaunti ya You tube ya Nisher yenye jina la Nisher Bybee, Adam alichukua muda wake kuitazama video mpya ya G-Nako na Ben Pol 'Mama Yeyo' na kuandika comments zake juu ya video hiyo pamoja na ushauri wa jumla kwa kazi za Nisher.
Adam alianza kwa kutoa credit kwa video ya Mama Yeyo, na kisha kumshauri Nisher kurekebisha baadhi ya vitu vya kitaalam katika uandaaji wa videos zake, na mwisho akamsifia "Yes you have talent, groom it to the direction with knowledge and you will surpass anything", ndivyo Adam alivyo m-salute Nisher.
Soma comments za Adam Juma na majibu ya Nisher kwake.
0 comments:
Post a Comment