Katika hali isiyo ya kawaida watu watatu ambao wote ni wanatoka United Arab Emirates (UAE), walitolewa kwa nguvu na polisi wa kidini katika tamasha lilijulikana kama ‘Jenadrivah Heritage and Culture Festival’ lililofanyika Riyadh mji mkuu wa Saudi arabia kwa hofu kuwa wanawake wangeshawishika sana kutokana na mvuto wa mmoja wao ambae waliambatana nae alitambulika kwa jina la Omar Borkan Al Gala.
Picha za kijana huyo handsome zimeonekana baada ya gazeti la kiarabu ‘Elaph’ kuripoti na kulitaja jina lake.
Japokuwa hali yake ya mahusiano bado haijajulikana tukio hilo limemzulia mengi zaidi kijana huyo baada ya picha na uzuri wake kuwekwa hadharani kupitia vyombo vya habari.
Ukurasa wake wa facebook sasa umejaa mialiko mingi ya wanawake kutoka katika nchi mbalimbali duniani wakimuahidi kuwa katika nchi yao hatofukuzwa.
Lakini kama kawaida matapeli hutumia kila nafasi kupata kile wanachokitaka na tayari wameshafungua fan page nyingi zenye jina lake lakini yeye mwenyewe ameandika status kuwa ana account moja tu ya facebook.
Kupitia fan page yake halisi Omar Borkan Al Gala ameandika:
“Hi, and thank you for all those lovely messages. I'm sorry I haven't had time to get back to all of you Xoxo I Love you all !
nb: I dont Have another account
only Fb So other borkan's or other names with my pics are fake >>` trying to be unique”
Hii ni video ya inayoonesha jinsi jamaa alivyo handsome kweli:
0 comments:
Post a Comment