Saturday, August 10, 2013

Dawa za ‘digital’ zinazotuma ujumbe kwa daktari kutokea tumboni mwa mgonjwa!

Teknlojia imesaidia wataalamu kutengeneza dawa zinazoweza kutoa taarifa kwa daktari kutokea tumboni mara baada ya kumezwa ili kukabiliana na wagonjwa wanaokatisha dozi au matumizi ya kimakosa yanayoweza kuleta athari.
dawa-3
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani World Health Organisation (WHO), asilimia 50 ya wagonjwa huwa hawatumii dawa wanazopewa kwa usahihi na zaidi ya asilimia 50 ya dawa husambazwa au kuuzwa kimakosa.
Hali hiyo si tu inaweza kuwa na madhara ya kutisha kwa wagonjwa, pia inawagharamu mamilioni ya pesa watoa huduma ya afya ya kila mwaka.
Andrew Thomson CEO wa Proteus Digital Health ya California, Marekani alisema tatizo kubwa liko kwa wagonjwa wenye magonjwa sugu wanaotakiwa kumeza dawa kila siku na kwa usahihi, na kushindwa kufanya hivyo kuna hatarisha maisha ya mgonjwa. “And what we know is that most people don’t actually do that very well.” Alisema.
Kwa teknolojia ya dawa hizo za digitali sasa itakuwa rahisi kumfuatilia mgonjwa kama amemeza dawa na kwa usahihi kwa mujibu wa Proteus.
sensor
Sensor
Dawa hizo zinatengenezwa kwa kuwekewa sensor ndogo katikati ya kidonge na kufanya kazi kama betri ya viazi “Ukichukua kipande cha shaba na ‘magnesium’ ukaviunganisha kwenya viazi unauwezo wa kuwasha taa” alisema Thomson. (ingia hapa kuona jinsi viazi vinavyoweza kutoa nguvu kama bettry).
Aliendelea kusema “What we have done is to take two absolutely required dietary minerals, one is copper and one is magnesium, and put them on a grain of sand that’s less than a millimetre square in a way that means that when we combine it with a drug, when you swallow it you become a potato.”
“Effectively when you swallow one of our digital drugs it will say, Hello I’m here, I’m Novartis, I’m Diovan, 1.2mg, I’m from plant number 76, I’m batch number 12 and I’m pill number 2.” Alisema Mr Thomson.
dawa-2
Kampuni hiyo ya Proteus imedai kuwa teknolojia hiyo iliyofanyiwa majaribio nchini Uingereza kwenye duka la dawa la High Street chain Lloyds imetoa majibu ya uhakika kwa zaidi ya asilimia 99.
Toleo la app hiyo kwaajili ya wagonjwa ‘ MedSnap PT’ linategemewa kuzinduliwa mwaka 2014 na kuna mipango ya kutumia teknolojia hiyo pia kubaini dawa bandia.
Source: BBC

0 comments:

Post a Comment