Wakati watanzania wengi hususani wadau na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania wakiisubiri jumapili kuupokea mwili wa mpendwa wao Albert Mangwea aliyefariki katika Hospitali ya St. Hellen Afrika kusini, taarifa za uhakika zilizopatikana zinasema mwili huo utaingia Tanzania jumanne saa nane mchana na sio jumapili saa nane mchana kama ilivyotegemewa.
Ripoti zilizotolewa na mtangazaji wa Clouds FM Millard Ayo ambae yuko nchini humo akifuatilia na kuripoti kuhusu kile kinachoendelea zimethibitisha mabadiliko haya.
Millard ameandika kupitia ukurasa wake wa facebook, “#CloudsFM #SA Ni uhakika kwamba mwili wa Marehemu Albert Mangwea utaingia Dar es salaam wiki ijayo jumanne saa nane mchana kutokea hapa Johannesburg, unaweza kushea hii post mtu wangu na wengine wapate taarifa.”
Millard alifafanua hali iliyopelekea mabadili hayo na kusisitiza kuwa pesa sio kikwazo bali ni kutokana na taratibu za nchi hiyo ambazo bado hazijakamilishwa.
“#CloudsFM #SA Inaweza kuwa ngumu kuelewa lakini ungekuepo huku mtu wangu ungeelewa, hapa ni S.A LAZIMA KILA HATUA IFATWE, ingekua Tanzania najua isingechukua time lakini hii ni nchi nyingine watu wangu, nimeshuhudia kila hatua.. sio rahisi kama wengi tunavyodhani.. tatizo sio pesa.”
Pia Ripoti kutoka nchini humo zinasema afya ya msanii M 2The P aliyekuwa na marehemu Ngwair inaendelea kuimalika na kutia matumaini.
Kwa upande mwingine, Miraji Kikwete ambae ni mtoto wa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ametoa vazi rasmi litakalotumika kama moja ya ishara ya kumuenzi marehemu albert Mangwea. Vazi hilo ambalo ni T-shirt lina picha ya ya kuchorwa ya Ngwair na maandishi “R.I.P Ngwair”.
0 comments:
Post a Comment